Yanga itarudi ikiwa imara zaidi

Misimu miwili nyuma Yanga ilicheza fainali ya kombe la Shirikisho (CAF CC) na kukosa ubingwa kwa mujibu wa kanuni baada ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya USM Alger

Haya ni mafanikio makubwa zaidi ambayo Yanga wameyapa katika soka la Afrika katika kipindi cha miaka 20 iliyopita. Ni sahihi kusema Yanga ndio timu iliyofanikiwa zaidi kutoka Tanzania katika mashindano ya CAF katika kipindi hicho kwani wananchi wanayo medali ya mshindi wa pili kabatini

Msimu uliopita Wananchi wakafanikiwa kucheza robo fainali ya ligi ya mabingwa, pengine ulikuwa msimu ambao Yanga ingeweza kucheza nusu fainali kama sio kile walichofanyiwa Afrika Kusini katika mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns

Ni bahati mbaya msimu huu Yanga haikufikia kile walichofanya katika misimu miwili iliyopita, timu ikiondoshwa katika hatua ya makundi ligi ya mabingwa

Msimu huu Yanga iliweka malengo makubwa zaidi ya kufanya vizuri lakini unaweza kusema mwanzo mbaya katika mechi mbili za awali ulivuruga mipango ya Wananchi mapema

Kuna kazi kubwa imefanyika na benchi la ufundi chini ya kocha Sead Ramovic hadi timu kumaliza katika nafasi ya tatu kundi A ikikusanya alama 8

Licha ya kuanza vibaya, Yanga imefikia idadi ya alama ambazo walikusanya msimu uliopita na kufuzu robo fainali lakini hazikutosha msimu huu

Hichi kilichotokea msimu huu kinakwenda kutengeneza 'njaa' mpya ya mafanikio na tutarajie kuona Yanga ikiimarika na kuwa bora zaidi msimu ujao

Kwa sasa mkakati ni kuhakikisha ufalme wa ndani haupotei, ni lazima kutetea mataji yote ambayo Yanga inayashikilia yaani ligi kuu ya kombe la FA kwani tayari Ngao ya Jamii iko mikononi

Mikiki mikiki ya ligi kuu tanzania bara inatarajia kuendelea wikendi hii Usikose kuitazama mechi ya S YANGA ðŸ†š KAGERA SUGAR LIVE bure kupitia simu yako download App yetu mapema inayorusha mechi zote live bure pia ukiwa na App yetu utaweza kutazama chanel zote za Azam Tv na DSTV live bure mfano Azam sport 1, Azam Two, Sinema zetu na nyingine nyingi

Kudownload  Bonyeza hapa ili kudownload App

Au

Au Bonyeza hapa kudownload

Au hapa chini


App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK kisha uta Install kawaida tu na uendelee kufurahia chanel za Azam na Dstv bureee ( ikileta neno its harmful usiogope ni kwasababu haijawekwa playstore)

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post