Ushindi ni lazima dhidi ya CS Constantine - Camara

Mlinga lango namba moja wa Simba Moussa Camara amesema watahakikisha wanashinda mchezo dhidi ya CS Constantine utakaopigwa Jumapili katika uwanja wa Benjamin Mkapa ili kumaliza hatua ya makundi CAF CC wakiwa kileleni kundi A

Simba tayari inayo mkononi tiketi ya robo fainali kombe la Shirikisho ikikusanya alama 10 kundi A baada ya kushuka dimbani mara 5

CS Constantine wanaongoza kundi A wakiwa na alama 12, hivyo Simba inahitaji ushindi wa aina yoyote Jumapili ili kuwapiku miamba hao kutoka Algeria katika nafasi ya kwanza

Camara amesema hesabu za kumaliza kinara wa kundi zina umuhimu mkubwa kwani itawasaidia katika hatua ya robo fainali kuanzia ugenini na kumalizia nyumbani

"Tumefuzu robo fainali lakini tuna mambo muhimu ambayo tunapaswa kuyakamilisha. Tunataka kushinda hii mechi ya mwisho dhidi ya Constantine ili tuongoze kundi letu jambo ambalo litatupa faida huko tunakokwenda"

"Endapo tukifanikiwa kushinda tutacheza mechi za robo fainali tukianzia ugenini na kumalizia nyumbani, kama mnavyoona hakuna timu ambayo imefanikiwa kuondoka hata na pointi moja tukiwa nyumbani hii ina maana tutapata nafasi ya kuja kumalizia vizuri mchezo wa robo na hata kwenda nusu fainali"

"Hatusahau kwamba hii ni timu ambayo ilitufunga kwao, hakuna timu nyingine iliyoondoka na pointi tatu dhidi yetu, tunataka kusahihisha makosa yetu, walipata ushindi ule kwa makosa yetu, tutakuwa nyumbani kusahihisha makosa yetu," alisema Camara

🤔Bado hujadownload App ya kuangalia Mechi hizi?🤔

Usikose kuitazama mechi ya YANGA ðŸ†š MC ALGER na SIMBA 🆚 CS COSTANTINE LIVE bure kupitia simu yako download App yetu mapema inayorusha mechi zote live bure pia ukiwa na App yetu utaweza kutazama chanel zote za Azam Tv na DSTV live bure mfano Azam sport 1, Azam Two, Sinema zetu na nyingine nyingi

Kudownload  Bonyeza hapa ili kudownload App

Au


App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK kisha uta Install kawaida tu na uendelee kufurahia chanel za Azam na Dstv bureee ( ikileta neno its harmful usiogope ni kwasababu haijawekwa playstore)

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post