USAJILI Uliokamilika dirisha dogo la Usajili 2024/2025
Tunakueletea orodha ya sajili zilizokamilika Katika dirisha hili dogo la usajili Msimu wa 2024/2025.
Dirisha hilo lilifunguliwa tarehe 15 December 2024 na limefungwa tarehe 15 January 2025.
Klabu ya Singida Black Stars imekamilisha usajili wa aliyekuwa Kiungo mshambuliaji, Serge Pokou mwenye umri wa miaka miaka 24 Kutoka Al Hilal Omdurman SC ya Sudan.
Klabu ya Young Africans imekamilisha usajili wa winga, Jonathan Ikangalombo mwenye umri wa miaka 22 Kutoka AS Vita Club ya kwao DR Congo.
Klabu ya Tabora United imekamilisha usajili wa Kiungo wa ulinzi ‘Cedric Martial Zemba’ raia wa Cameroon mwenye umri wa miaka 25 kutoka Klabu ya Soka ya Tourga ya nchini Morocco.
Klabu ya KenGold FC imekamilisha usajili wa beki wa zamani , Steven Duah Namungo FC na Kagera Sugar Duah.
Klabu hiyo pia imekamilisha usajili wa Kiungo Mshambuliaji wa zamani wa Vilabu vya Simba na Yanga, Benard Morrison Kwa mkataba wa miezi sita.
Klabu ya Namungo FC imekamilisha usajili wa Mshambuliaji, Saleh Karabaka Kwa Mkopo wa miezi sita Kutoka Simba SC
Klabu ya Singida Black Stars imekamilisha usajili wa, beki Frank Kwabena Assinki raia wa Ghana mwenye umri wa miaka 22 kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka HB Køge ya Denmark ambayo ilimtoa kwa mkopo KFUM Roskilde tangu mwaka 2021.
Klabu ya KenGold FC imekamilisha usajili wa Kiungo Mshambuliaji, Lassa Gradi Kiala raia wa DR Congo mwenye umri wa miaka 26 Kwa mkataba wa miezi sita Kutoka Zanaco FC.
Beki Israel Patrick Mwenda amejiunga na Young Africans kutoka Singida Black Stars Kwa Mkopo wa miezi sita.
Kiungo Mshambuliaji, Deus David Kaseke amejiunga na Pamba Jiji FC ya Mwanza kama Mchezaji huru.
Beki Sandale Komanje amejiunga na Ken Gold akitokea Tabora United FC ya Mkoani Tabora.
Emmanuel Mwanengo amejiunga na Tabora United ya Tabora kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Mwanengo amejiunga na Tabora United kama mchezaji huru baada ya mkataba wake na Vakhsh ya nchini Tajikistan kumalizika.
Hamadi Majimengi amejiunga na Pamba Jiji kwa mkopo wa miezi sita Kutoka Singida Black Stars.
Klabu ya Namungo FC, imefanikiwa kumrejesha aliyewahi kuwa beki wao Derick Mkombozi raia wa Burundi.
Mshambuliaji, Habibu Hajii Kyombo amejiunga na klabu ya Pamba Jiji ya Jijini Mwanza.
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Yanga Yusuf Athumani amejiunga na klabu ya Fountain Gate kwa mkataba wa mwaka mmoja kama mchezaji huru
Usikose kuitazama mechi ya YANGA 🆚 MC ALGER LIVE bure kupitia simu yako download App yetu mapema inayorusha mechi zote live bure pia ukiwa na App yetu utaweza kutazama chanel zote za Azam Tv na DSTV live bure mfano Azam sport 1, Azam Two, Sinema zetu na nyingine nyingi
Kudownload Bonyeza hapa ili kudownload App
Post a Comment