TP Mazembe imekuwa timu ya kwanza kutupwa nje ya michuano ya ligi ya mabingwa kundi A baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa MC Alger hapo jana
Mazembe walihitaji kushinda mchezo huo uliopigwa Algeria jana lakini bao la mkwaju wa penati kipindi cha kwanza liliwapa MC Alger alama tatu nyumbani na kuwakatia Mazembe tiketi ya kurudi nyumbani
Matokeo hayo pia yanamaanisha Yanga haipaswi kupoteza mchezo dhidi ya Al Hilal hapo kesho ili kuweka hai matumaini ya kufuzu robo fainali
Al Hilal inayoongoza kundi A ikiwa alama 10, tayari imefuzu huku MC Alger wakiendelea kushikilia nafasi ya pili wakiwa na alama 8
Yanga ni ya tatu ikiwa na alama 4 wakati TP Mazembe wanaburuza mkia wakiwa na alama 2
Kama Yanga itapoteza mchezo dhidi ya Al Hilal hapo kesho, itaungana na TP Mazembe kuondoshwa katika michuano hiyo kwani hata ikishinda mechi ya mwisho dhidi ya MC Alger itafikisha alama 7 ambapo tayari MC Alger wana alama 8
Yanga inahitaji kushinda mechi mbili zilizobaki ili kufuzu robo fainali moja kwa moja na kama ikitoka sare dhidi ya Al Hilal, itahitaji kupata ushindi wa kuanzia mabao 3-0 dhidi ya MC Alger ili kufuzu
usikose kuitazama mechi ya AL HILAL 🆚 YANGA na BRAVO 🆚 SIMBA LIVE bure kupitia simu yako download App yetu mapema inayorusha mechi zote live bure pia ukiwa na App yetu utaweza kutazama chanel zote za Azam Tv na DSTV live bure mfano Azam sport 1, Azam Two, Sinema zetu na nyingine nyingi
Kudownload Bonyeza hapa ili kudownload App
Post a Comment