Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali amesema kikosi kinaendelea vyema na maandalizi na mpaka sasa hawajakumbana na hujuma za aina yoyote
CS Sfaxien itawakaribisha Simba katika mechi ya raundi ya nne ya Kundi A itakayochezwa kesho kuanzia saa 1:00 usiku kwa saa za Tanzania kwenye Uwanja wa Olympique Hammadi Agrebi
Katika mchezo uliozikutanisha timu hizo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, mashabiki wa CS Sfaxien walianzisha vurugu kufuatia Simba kupata bao la dakika za 'jioni' lililofungwa na Kibu Denis, wenyeji wakapata ushindi wa mabao 2-1, ambapo viti kadhaa vya uwanja huo viling'olewa
Ahmed amesema mashabiki na wanachama wa klabu hiyo wasiwe na wasiwasi wowote kwa sababu walitua Tunisia salama na hawakukutana na changamoto yoyote kuanzia kwenye uwanja wa ndege hadi hotelini, sehemu ambazo mara nyingi dalili za figisu za soka huanzia hapo
Ahmed alisema wamejitahidi kukwepa kila eneo ambalo wanadhani wangeweza kufanyiwa hujuma kwa kushirikiana na ubalozi wa Tanzania nchini Tunisia
"Tuliwasili salama baada ya safari ndefu, hakuna changamoto yoyote, shauku imekuwa ni kubwa na hofu imekuwa kubwa hasa kwa Wanasimba wakioanisha na kile ambacho kilitokea katika mechi ya kwanza, pengine wakidhani ingeweza kutusumbua baada ya kufika hapa, niwaambie kila kitu kimekwenda vizuri"
"Muda tuliokaa uwanja wa ndege ni ule ambao unatumiwa na viwanja vyote, maana yake hakukuwa na vigisu yoyote ile, lakini haya yote tumeyafanya kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Tunisia, kila kitu kimekwenda vizuri," alisema Ahmed
Kuhusu hali ya hewa, Ahmed alisema ni baridi lakini siyo kama ile waliyokutana nayo nchini Algeria walipokwenda kucheza dhidi ya CS Constantine
Naye nahodha msaidizi wa timu hiyo, Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' amesema wachezaji wote wako katika hali nzuri na wanatarajia kupambana kuhakikisha wanapata matokeo chanya
"Tumekuja kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho ndani ya uwanja kwa dakika 90, hatuna hofu, mpaka sasa hakuna chochote, najua hakuna chochote kibaya kitakachotokea, pia sisi hatuogopi chochote, ni wazoefu sana katika michuano ya kimataifa na tumeshakutana na mambo mengi ndani na nje ya uwanja"
"Sisi tumekuja kucheza mpira, hayo mambo mengine huwa yanatokea tu bila kupangwa, ukiangalia hata siku ile mashabiki wao walianzisha vurugu kwa sababu hawakupata matokeo waliyotarajia ya sare ambayo tayari wao walishajua wameipata," alisema beki huyo
CS Sfaxien imepigwa marufuku kuingiza mashabiki kutokana na kufanya fujo katika mchezo wao dhidi ya CS Constantine ambao walipoteza kwa kufungwa bao 1-0, mechi iliyochezwa Novemba 27, mwaka jana
Huenda klabu hiyo ikakumbana na rungu lingine kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), kufuatia baadhi ya viongozi wa benchi la ufundi, wachezaji na mashabiki kufanya vurugu katika mchezo dhidi ya Simba uliochezwa Desemba 15, mwaka jana
Baada ya mechi hiyo, Simba itajipanga kuwafuata Bravos do Maquis na itamaliza mechi za hatua ya makundi nyumbani kwa kuwakaribisha CS Constantine kutoka Algeria.
Usikose kuitazama mechi ya YANGA 🆚 TP MAZEMBE na CS SFAXIEN 🆚 SIMBA LIVE bure kupitia simu yako download App yetu mapema inayorusha mechi zote live bure pia ukiwa na App yetu utaweza kutazama chanel zote za Azam Tv na DSTV live bure mfano Azam sport 1, Azam Two, Sinema zetu na nyingine nyingi
Kudownload Bonyeza hapa ili kudownload App
Au
App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK kisha uta Install kawaida tu na uendelee kufurahia chanel za Azam na Dstv bureee
Post a Comment