Simba na CS Constantine zimejiweka katika nafasi nzuri ya kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho (CAF CC) baada ya kushinda mechi zao za raundi ya nne
Ikicheza ugenini huko Tunisia Simba iliichapa CS Sfaxine bao 1-0 na kufikisha alama 9 ambapo kimahesabu inahitaji angalau alama moja tu kutoka mechi mbili zilizobaki ili iweze kufuzu robo fainali
CS Constantine waliibamiza Bravos mabao 4-0 huko Algeria nao wakifikisha alama 9 na kurejea kileleni mwa kundi A wakiwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa
Mchezo unaofuata kwa Simba ni dhidi ya Bravos utakaopigwa wiki ijayo huko Angola
Pengine huu ndio mchezo ambao Simba inaweza kujihakikishia kutinga robo fainali kama haitapoteza
Bravos wako nafasi ya tatu wakiwa na alama 6, kama watakosa ushindi dhidi ya Simba maana yake ni kuwa hawataweza kuwa juu ya Simba kwenye msimamo sababu ya 'H2H' yaani Simba imepata matokeo mazuri timu hizo zilipokutana
Usikose kuitazama mechi ya AL HILAL 🆚 YANGA na BRAVO 🆚 SIMBA LIVE bure kupitia simu yako download App yetu mapema inayorusha mechi zote live bure pia ukiwa na App yetu utaweza kutazama chanel zote za Azam Tv na DSTV live bure mfano Azam sport 1, Azam Two, Sinema zetu na nyingine nyingi
Kudownload Bonyeza hapa ili kudownload App
Post a Comment