Wakati dirisha dogo la usajili likitarajiwa kufungwa kesho Jumatano, Januari 15, Simba ni kama imefunga hesabu zake katika dirisha hili kwa usajili wa Elie Mpanzu
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Simba imedokeza kuwa kocha Fadlu Davids amefunga hesabu zake katika dirisha hili
Katika moja ya mahojiano yake, Fadlu aliweka wazi ugumu wa kupata aina ya wachezaji anaowahitaji ambao wanapaswa kuingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza kama ilivyokuwa kwa Mpanzu
"Hatutafanya usajili mkubwa katika dirisha dogo kwa sababu katika kipindi hiki ni ngumu kuwapata aina ya wachezaji ambao tunawahitaji"
"Wakati huu wachezaji wanakuwa na mikataba na timu zao zinaweka masharti magumu kuwauza hasa wanapokuwa wanategemewa"
"Unaposajili mchezaji kipindi hiki ni muhimu kuhakikisha ana sifa ya kuingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza kama ilivyokuwa kwa Mpanzu," alisema Fadlu
Katika dirisha hili Simba imehusishwa kumuwania kiungo wa Azam Fc Feisal Salum 'Fei Toto', hata hivyo imekuwa sio rahisi kwa Azam Fc kusikiliza ofa ya Simba kwa kuwa bado wanamuhitaji mchezaji huyo
Lakini pia Simba iliulizia upatikanaji wa kiungo wa Vipers Fc ya Uganda Allan Okello. Vipers Fc wamekuwa wagumu kufanya biashara na Simba tangu wakati wa mshambuliaji Cesar Manzoki
Inavyoonekana mpaka sasa hakuna matarajio ya ingizo jipya labda itokee 'surprise' kama ambavyo Simba imekuwa ikifanya katika kila dirisha
Usikose kuitazama mechi ya YANGA 🆚 MC ALGER na SIMBA 🆚 CS COSTANTINE LIVE bure kupitia simu yako download App yetu mapema inayorusha mechi zote live bure pia ukiwa na App yetu utaweza kutazama chanel zote za Azam Tv na DSTV live bure mfano Azam sport 1, Azam Two, Sinema zetu na nyingine nyingi
Kudownload Bonyeza hapa ili kudownload App
Post a Comment