Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic amesema hakuna matokeo mengine ambayo yatakuwa na maana kwao zaidi ya ushindi katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya MC Alger ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Akizungumza katika Mkutano na wanahabari mapema leo, Ramovic alisema ameandaa mkakati maalum wa kimbinu kuikabili MC Alger katika mchezo ambao ushindi ni matokeo ya lazima kwao
"Tunahitaji ushindi katika mchezo huo. Tunajua tunakwenda kucheza mechi ngumu dhidi ya MC Alger, tumejiandaa vyema, tumeandaa mpango wetu wa mchezo huu, tunataka kushinda ili tuwape furaha mashabiki wetu na wale wanaotuunga mkono"
"Kila mmoja anajua umuhimu wa mchezo huu, sio kwetu tu tunajua hata wapinzani wetu wanajua wanahitaji nini, nina matumaini makubwa kutokana na namna wachezaji wangu wanajitoa na kuelewa mfumo wangu, kesho tunakwenda kujitoa kwa kila iwezekanavyo"
"Tunakwenda kulipuka kama moto kuhakikisha tunaweka utawala katika mchezo huo, " alisema Ramovic
Ramovic amethibitisha atamkosa Maxi Nzengeli ambaye licha ya kuanza mazoezi na timu, bado hayuko tayari kucheza
Beki Yao Kouassi nae atakosekana akiwa amefanyiwa upasuaji wa goti na anaweza kuwa nje hadi wiki 6
Yanga inahitaji ushindi wa aina yoyote ili kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa kwa msimu wa pili mfululizo
🤔Bado hujadownload App ya kuangalia Mechi hizi?🤔
Usikose kuitazama mechi ya YANGA 🆚 MC ALGER na SIMBA 🆚 CS COSTANTINE LIVE bure kupitia simu yako download App yetu mapema inayorusha mechi zote live bure pia ukiwa na App yetu utaweza kutazama chanel zote za Azam Tv na DSTV live bure mfano Azam sport 1, Azam Two, Sinema zetu na nyingine nyingi
Kudownload Bonyeza hapa ili kudownload App
Post a Comment