Wakati klabu ya MC Alger ikitoa taarifa ya kutua nchini Alfajiri ya kuamkia Alhamisi, imebainika tayari baadhi ya wachezaji na maafisa wa klabu hiyo wameingia nchini
Baadhi ya wachezaji waliwasili juzi wakiwa katika kundi la kwanza lililojumuisha mashabiki wa timu hiyo
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema Yanga haijali MC Alger wanakuja kwa utaratibu gani lakini muhimu wahakikishe Jumamosi wametimia pale uwanja wa Benjamin Mkapa
"Walitoa taarifa kuwa watawasili nchini Alfajiri ya kuamkia Alhamisi lakini kwa kuwa Yanga ni timu kubwa tumebaini tayari baadhi yao wameshafika"
"Sisi tunawaambia hatujali wanakuja kwa utaratibu gani, hata kama watapanda Ngamia sawa tu lakini muhimu wahakikishe Jumamosi wako pale uwanja wa Benjamin Mkapa tena wakiwa wametimia," alitamba Kamwe
Baada ya kurejea kutoka Mauritania jana, kikosi cha Yanga leo kinaanza maandalizi ya mwisho ya mchezo huo utakaopigwa Jumamosi, Januari 18 saa 10 jioni
Usikose kuitazama mechi ya YANGA 🆚 MC ALGER LIVE bure kupitia simu yako download App yetu mapema inayorusha mechi zote live bure pia ukiwa na App yetu utaweza kutazama chanel zote za Azam Tv na DSTV live bure mfano Azam sport 1, Azam Two, Sinema zetu na nyingine nyingi
Kudownload Bonyeza hapa ili kudownload App
Post a Comment