Mechi za raundi ya tano hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika zinaanza kutimua vumbi leo ambapo mechi moja ya kundi A itapigwa huko Algeria
Wenyeji MC Alger wataikaribisha TP Mazembe katika mchezo ambao matokeo yake yatafuatiliwa kwa karibu na mashabiki wa Yanga
TP Mazembe wataaga rasmi michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu kama watakosa ushindi leo wakati MC Alger kama hawatashinda mchezo huo wataipa ahueni Yanga kuelekea mchezo dhidi ya Al Hilal utakaopigwa Jumapili
Kwa kuzingatia msimamo wa kundi ulivyo, MC Alger wanashika nafasi ya pili wakiwa na alama 5, kama watashinda dhidi ya Mazembe watafikisha alama 8 na kuilazimu Yanga kuhakikisha haipotezi mchezo dhidi ya Al Hilal ili kuendelea kubaki katika kinyang'anyiro cha kuwania tiketi ya robo fainali
Kama MC Alger watatoka sare dhidi ya Mazembe leo maana yake Yanga itahitaji kushinda mchezo wa mwisho dhidi ya MC Alger ili kutinga robo fainali pasipo kujali matokeo ya mchezo dhidi ya Al Hilal
Ikitokea TP Mazembe wameshinda dhidi ya MC Alger leo, itailazimu Yanga kuhakikisha inakusanya alama 4 kutoka mechi mbili zilizobaki ili kutinga robo fainali
Akizungumza na wanahabari muda mfupi kabla ya kuelekea Mauritania jana, Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic alisisitiza kuwa malengo ya Yanga ni kuhakikisha wanashinda mechi zote mbili zilizobaki ili kufuzu robo fainali pasipo kujali matokeo ya wapinzani wao
pia usikose kuitazama mechi ya AL HILAL 🆚 YANGA na BRAVO 🆚 SIMBA LIVE bure kupitia simu yako download App yetu mapema inayorusha mechi zote live bure pia ukiwa na App yetu utaweza kutazama chanel zote za Azam Tv na DSTV live bure mfano Azam sport 1, Azam Two, Sinema zetu na nyingine nyingi
Kudownload Bonyeza hapa ili kudownload App
Post a Comment