Hatimaye ile siku imewadia! Nyasi za uwanja wa Benjamin Mkapa zitawaka moto leo pale mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga ambao ni wawakilishi pekee wa nchi katika michuano ya ligi ya mabingwa watakapomenyana na TP Mazembe
Ni mechi ya kuamua hatma ya Yanga katika michuano hiyo. Wananchi wanahitaji ushindi tu ili kuweka hai matumaini ya kufuzu robo fainali
Kwa aina ya maandalizi ambayo kikosi cha kocha Sead Ramovic kimefanya, ni wazi mechi ya leo itakuwa kama fainali
Pamoja na ugumu wa TP Mazembe, hakuna namna Wacongoman hao hawapaswi kutoka salama dimba la Mkapa
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuhakikisha wanaujaza uwanja wa Mkapa
Kamwe amesema kwa heshima ya Yanga, haipaswi kuwa katika nafasi waliyopo katika msimamo wa kundi A
"Mechi hii ni sio ya wachezaji pekee, bali ni ya kila shabiki na Mwanachama wa Yanga. Tujitokeze kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa kushuhudia Gusa achia twende kwao ya Kimataifa"
"Kwa wale ambao hamtaweza kufika dimba la Mkapa, kila mmoja na imani yake, afanye maombi ili tuweze kushinda mchezo huu," alisma Kamwe
Kila la kheri Wananchi...!
Usikose kuitazama mechi ya YANGA 🆚 TP MAZEMBE na CS SFAXIEN 🆚 SIMBA LIVE bure kupitia simu yako download App yetu mapema inayorusha mechi zote live bure pia ukiwa na App yetu utaweza kutazama chanel zote za Azam Tv na DSTV live bure mfano Azam sport 1, Azam Two, Sinema zetu na nyingine nyingi
Kudownload Bonyeza hapa ili kudownload App
Au
App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK kisha uta Install kawaida tu na uendelee kufurahia chanel za Azam na Dstv bureee
Post a Comment