Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga leo wanatupa karata muhimu katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAF CL) pale watakapoumana na MC Alger katika mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi
Dakika 90 za mchezo huo zinabeba hatma na matarajio ya Yanga kucheza robo fainali kwa msimu wa pili mfululizo
Ni ushindi pekee ambao utaipa Yanga nafasi ya kufuzu robo fainali huku wapinzani wao wakihitaji sare tu
Unaweza kusema leo pale dimba la Mkapa yanahitajika matokeo ya aina moja tu, Yanga ishinde au MC Alger wapoteze na si vinginevyo
Hii ni mechi ya kuiheshimisha Yanga katika mashindano ya CAF msimu huu kwani kama watafanikiwa kutinga robo fainali, watapanda hadi nafasi ya tano katika 'ranking' za CAF na kuwapiku watani zao Simba ambao kwa miaka kadhaa sasa wamekuwa wakitambia nafasi yao CAF
Kwa wachezaji hii ni mechi yenye thamani kubwa kwani ushindi utawahakikishia kuvuna kiasi kikubwa che fedha. Endapo Yanga itatinga robo fainali, itakuwa na uhakika wa kuvuna zaidi ya Tsh bilioni 2.3
🤔Bado hujadownload App ya kuangalia Mechi hizi?🤔
Usikose kuitazama mechi ya YANGA 🆚 MC ALGER na SIMBA 🆚 CS COSTANTINE LIVE bure kupitia simu yako download App yetu mapema inayorusha mechi zote live bure pia ukiwa na App yetu utaweza kutazama chanel zote za Azam Tv na DSTV live bure mfano Azam sport 1, Azam Two, Sinema zetu na nyingine nyingi
Kudownload Bonyeza hapa ili kudownload App
Post a Comment