Klabu ya Kagera Sugar imewasilisha maombi rasmi kwa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga wakimuhitaji winga Denis Nkane kwa mkopo
Nkane amekuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kwa takribani misimu mitatu, ingawa nafasi yake katika kikosi cha kwanza ni finyu
Mtendaji Mkuu wa Kagera Sugar Thabiti Kandoro amethibitisha kumuhitaji mchezaji huyo
"Ni kweli suala hilo lipo lakini hatuwezi kulizungumzia kwa sababu mchakato bado haujakamilika. Mambo yakienda kama yalivyopangwa taarifa itatolewa," alisema Kandoro
Katika dirisha hili dogo la usajili, Yanga imemsajili mlinzi kiraka Israel Mwenda huku ikihusishwa na winga Jonathan Ikangalombo sajili ambazo huenda zikafanya nafasi ya Nkane kuwa finyu zaidi
Wakati Yanga ikinolewa na Miguel Gamondi, mara kadhaa Nkane alitumika kama mlinzi wa kulia lakini tangu ujio wa Sead Ramovic, nafasi hiyo anatumika zaidi Kibwana Shomari huku Nkane akitumika kama winga katika baadhi ya mechi
Mara kadhaa Rais wa Yanga Injinia Hersi Said ameweka wazi kuwa wana malengo ya muda mrefu na Nkane
AL HILAL 🆚 YANGA na BRAVO 🆚 SIMBA LIVE bure kupitia simu yako download App yetu mapema inayorusha mechi zote live bure pia ukiwa na App yetu utaweza kutazama chanel zote za Azam Tv na DSTV live bure mfano Azam sport 1, Azam Two, Sinema zetu na nyingine nyingi
Kudownload Bonyeza hapa ili kudownload App
Post a Comment