Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic juzi alimfanyia mabadiliko Stephane Aziz Ki dakika 5 tu baada ya kuanza kipindi cha pili cha mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc uliopigwa uwanja wa Majaliwa, Ruangwa na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0
Clatous Chama ndiye aliyeingia kuchukua nafasi ya Aziz Ki na kwa kiasi kikubwa Chama aliongeza kasi ya mashambulizi akitoa pasi ya bao la pili lililofungwa na Pacome Zouzoua
Kilichowafurahisha wengi ni jinsi Chama alivyokuwa akiongoza kufanya 'pressing' dhidi ya walinzi wa Namungo Fc, yakiwa ni mabadiliko makubwa ya aina ya uchezaji wake
Akizungumzia sababu ya mabadiliko aliyofanya mapema kwa kumtoa Aziz Ki, Ramovic alisema kila mchezaji anahitaji kufanya kazi timu inapokuwa na mpira na hata bila ya mpira
Ramovic alisisitiza falsafa yake ni kushambulia na kuzuia kwa pamoja kuwanyima wapinzani nafasi ya kumiliki mpira kwa muda mrefu
"Aziz Ki alifanya kazi nzuri katika kipindi cha kwanza hasa timu inapokuwa haina mpira, tunataka kuona kila mchezaji anashiriki kikamilifu pale tunapotafuta mpira"
"Chama alipoingia nae amefanya kazi nzuri, ametengeneza bao la pili, hawa ni wachezaji wa daraja la juu ambao najivunia kuwa nao katika kikosi," alisema
Juzi Yanga ilionyesha mabadiliko ya kiuchezaji hasa ilipokuwa haina mpira. Mawinga na viungo wote walirudi chini kuzuia na kushambulia kwa haraka walipopata mpira
Mabao yote mawili yalikuwa ni matokeo ya 'transition' baada ya Yanga kupora mpira na kushambulia kwa haraka
Kennedy Musonda alifunga bao la kwanza baada ya pasi ya Maxi Nzengeli, mashambulizi yakianzia kwa Pacome Zouzoua aliyepora mpira upande wa kulia
Bao la pili alilofunga Pacome lilianzia nyuma ambapo Pacome alishiriki tena katika ulinzi kabla ya kutoa pasi kwa Duke Abuya ambaye alimpasia Chama aliyemtengea Pacome aliyekimbia kutoka nyuma na kufunga bao bora la mchezo huo
Usikose kuitazama mechi ya CS CONSTANTINE 🆚 SIMBA na MC ALGER 🆚 YANGA Live buree kupitia simu yako download App yetu ili kutazama mechi hii pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv mfano Azam two, Sinema zetu na nyingine nyingi
Kudownload Bonyeza hapa ili kudownload App
Au
App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK kisha uta Install kawaida tu na uendelee kufurahia chanel za Azam na Dstv bureee
Post a Comment