Yanga kuanza na Mashujaa kesho kutwa KMC Complex

Baada ya ombi la kubadili uwanja kutoka Azam Complex kwenda KMC Complex kukubaliwa na Bodi ya Ligi, keshokutwa Alhamisi, Disemba 19 Yanga itacheza mechi yake ya kwanza katika uwanja huo dhidi ya Mashujaa Fc

Wananchi wa Dar sasa watashuhudia mechi za timu yao mapema kwani mechi zote zinazochezwa KMC Complex zinaanza saa 10 jioni

Itakuwa mechi ya pili kwa kocha mkuu wa Yanga Sead Ramovic ambaye aliiongoza Yanga kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo Fc katika mchezo uliopita wa ligi

Mechi nyingine muhimu kwa Yanga kushinda ili kusogea katika nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki wa timu hiyo kuwa wamoja ili kuhakikisha wanashinda mechi zote nne za ligi zinazofuata kabla ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya TP Mazembe utakaopigwa Januari 03 2025 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Baada ya mchezo dhidi ya Mashujaa Fc, Disemba 22 Yanga itashuka tena uwanja wa KMC Complex kuikabili Tanzania Prisons kisha kusafiri jijini Dodoma kuikabili Dodoma Jiji Disemba 25

Disemba 29 Yanga itarejea tena KMC Complex kuikabili Fountain Gate

Usikose kuitazama mechi ya SIMBA 🆚 KEN GOLD na YANGA 🆚 MASHUJAA Live buree kupitia simu yako download App yetu ili kutazama mechi hii pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv mfano Azam two, Sinema zetu na nyingine nyingi

Kudownload  Bonyeza hapa ili kudownload App

Au


App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK kisha uta Install kawaida tu na uendelee kufurahia chanel za Azam na Dstv bureee


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post