Wachezaji Yanga 'wampagawisha' Ramovic

 

Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic ameeleza furaha yake baada ya kiwango kizuri kilichoonyeshwa na wachezaji wake katika mechi nne zilizopita

Akizungumza baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Fountain Gate, Ramovic alisema haikuwa rahisi kwao kucheza mechi nne ndani ya muda wa siku 10 na kilichomfurahisha ni jinsi wachezaji wake walivyopambana katika mechi hizo

"Kwa kweli najivunia kuwa katika timu hii yenye wachezaji wa kipekee. Nawapongeza sana kwa kazi nzuri waliyofanya siku ya leo (jana) lakini pia katika mechi zilizopita"

"Tumecheza mechi nne ndani ya siku 10, haikuwa rahisi lakini wachezaji wamepambana na kwa kiasi kikubwa wamefanya vile tunapaswa kucheza"

"Kushinda mabao 5 dhidi ya timu ngumu tena tukiwa tumetoka kucheza mechi nyingine ngumu sio kitu rahisi"

"Wakati nafika hapa wiki tano zilizopita nilisema tunahitaji wachezaji wawe 'fit' ili kuweza kucheza aina ya soka la kasi na kuwanyima wapinzani muda wa kupumua"

"Bado hatujafikia malengo kwa asilimia 100 lakini tumepiga hatua kubwa, hivyo niwapongeze pia wenzangu katika benchi la ufundi kwani kwa pamoja tumefanya kazi nzuri mpaka sasa," alisema Ramovic

Katika siku 10 Yanga imeshinda mechi nne dhidi ya Mashujaa (3-2), Prisons (4-0), Dodoma Jiji (4-0) na Fountain Gate (5-0)

Mabao ya kufunga ni 16 huku Wananchi wakiruhusu nyavu zao kutikiswa mara mbili tu

Usikose kuitazama mechi ya YANGA 🆚 TP MAZEMBE na CS SFAXIEN 🆚 SIMBA LIVE bure kupitia simu yako download App yetu mapema inayorusha mechi zote live bure pia ukiwa na App yetu utaweza kutazama chanel zote za Azam Tv na DSTV live bure mfano Azam sport 1, Azam Two, Sinema zetu na nyingine nyingi

Kudownload  Bonyeza hapa ili kudownload App

Au


App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK kisha uta Install kawaida tu na uendelee kufurahia chanel za Azam na Dstv bureee


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post