Usiichukulie Poa Yanga imepania kuzindukia kwa Mazembe

Usiichukulie Poa Yanga imepania kuzindukia kwa Mazembe

Usikose kuitazama mechi ya TP MAZEMBE 🆚 YANGA na SIMBA 🆚 CS SFAXIEN  Live buree kupitia simu yako download App yetu ili kutazama mechi hii pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv mfano Azam two, Sinema zetu na nyingine nyingi

Kudownload App Bonyeza hapa


Kesho Alhamisi kikosi cha Yanga kitasafiri kuelekea Lubumbashi DR Congo tayari kwa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya TP Mazembe

Mchezo huo wa raundi ya tatu hatua ya makundi, utapigwa Jumamosi, Disemba 14 saa 10 jioni katika uwanja wa Mazembe

Habari njema ni kuwa katika mchezo huo huenda baadhi ya nyota waaliokosekana katika mechi zilizopita kutokana na majeraha wakarejea

Khalid Aucho, Clement Mzize na Chadrack Boka sasa wameimarika wakishiriki kikamilifu mazoezi ya timu kama ilivyo kwa nahodha msaidizi Dickson Job aliyekuwa akisumbuliwa na maumivu ya goti

Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic amesema kurejea kwa wachezaji hao ni muhimu kuelekea mchezo huo wa ugenini ambao wanahitaji ushindi ili kufufua matumaini ya kufuzu robo fainali CAF CL

"Tangu nimefika hawa wachezaji (Boka, Aucho na Mzize) hawakuwa sawa nadhani kwa maendeleo yao tuna nafasi kubwa kuwaona wakicheza mechi ijayo, itakuwa ni kitu kizuri kuona nguvu yao inarudi kuungana na wenzao, pia Job anaweza kuwa tayari pia," alisema Ramovic

Ramovic amesema anaimani na kikosi chake, kupoteza mech mbili za mwanzo hayakuwa matarajio yake sasa wanapaswa kuamka ili kubadilisha mambo

"Tuna timu nzuri bahati mbaya hapa ni kwamba hizi mechi mbili za ligi ya mabingwa tumekosa matokeo mazuri, kila mmoja inamuumiza lakini sasa tunatakiwa kuamka kwa haraka na kubadilisha mambo," alisema Ramovic

Usikose kuitazama mechi ya TP MAZEMBE 🆚 YANGA Live buree kupitia simu yako download App yetu ili kutazama mechi hii pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv mfano Azam two, Sinema zetu na nyingine nyingi

Kudownload  Bonyeza hapa ili kudownload App

Au


App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK kisha uta Install kawaida tu na uendelee kufurahia chanel za Azam na Dstv bureee

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post