Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic amesema kikosi chake kiko tayari kwa mechi ngumu ya ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji ambayo itapigwa kesho Jumatano katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma
Akizungumza katika Mkutano na wanahabari, Ramovic alisema ameichambua Dodoma Jiji na kubaini ni timu ngumu hasa inapocheza katika uwanja wa Jamhuri hivyo watahitaji kucheza kwa tahadhari kubwa ili kupata alama 3
"Tumewatazama kwa makini sana Dodoma Jiji, wanacheza vizuri wakiwa nyumbani, tunafahamu ni wagumu mno wanapocheza nyumbani hivyo tumeshajiandaa kukabiliana nao. Alama tatu kesho muhimu mno kwetu ili tuendelee kubaki kwenye mipango yetu"
"Ushindi katika mchezo huo unabeba dhima nzima ya kujitoa kwa kila namna, kama tusipojitoa kwa kila hali hapo kesho matarajio ya ushindi yatakuwa madogo"
"Kimsingi tumekuja hapa na tumeshajiandaa kisawasawa na tuna imani ya kuondoka alama tatu. Bila shaka mchezo umekaa kimtego kutokana na ratiba lakini hiyo haiondoi dhamira yetu ya kushinda," alisema Ramovic
Aidha kocha huyo raia wa Ujerumani amesema atalazimika kufanya 'rotation' ya kikosi chake katika baadhi ya nafasi ili kuhakikisha anatunza nguvu ya kila mchezo kwa ajili ya mapambano katika mechi ambazo zinafuatana karibu karibu
Usikose kuitazama mechi ya DODOMA JIJI 🆚 YANGA na SIMBA 🆚JKT TANZANIA Live buree kupitia simu yako download App yetu mapema ili kutazama mechi hizi pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv mfano Azam two, Sinema zetu na nyingine nyingi
Kudownload Bonyeza hapa ili kudownload App
Au
App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK kisha uta Install kawaida tu na uendelee kufurahia chanel za Azam na Dstv bureee
Post a Comment