Tumejiandaa kucheza mechi ngumu Algeria - Fadlu

 Tumejiandaa kucheza mechi ngumu Algeria - Fadlu

Usikose kuitazama mechi ya CS CONSTANTINE 🆚 SIMBA na MC ALGER 🆚 YANGA Live buree kupitia simu yako download App yetu ili kutazama mechi hii pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv mfano Azam two, Sinema zetu na nyingine nyingi

Kudownload App Bonyeza Hapa


Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids amesema wamejiandaa kwa mechi ngumu dhidi ya CS Constantine ikiwa ni raundi ya pili ya hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC) 

Simba imeondoka nchini alfajiri ya leo Jumatano kuelekea Algeria wakipitia Uturuki tayari kwa mchezo huo utakaopigwa Jumapili, Disemba 08

Akizungumza na wanahabari muda mfupi kabla ya kuondoka uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, Fadlu alisema wamekamilisha maandalizi ya mchezo huo hapa nyumbani kazi iliyobaki ni kwa wachezaji kutekeleza mpango wa mechi hiyo hapo Jumapili

"Tumekamilisha maandalizi yetu ya kimbinu hapa nyumbani, Algeria tutafanya mazoezi ya kawaida kuelekea siku ya mchezo"

"Niseme tu tunakabiliwa na mechi ngumu dhidi ya CS Constantine. Ni timu nzuri ambayo inafanya vizuri kwa sasa. Walipata ushindi katika mechi yao ya kwanza ugenini"

"Ni lazima tuwe bora na kuepuka kufanya makosa ambayo yanaweza kutugharimu katika mchezo huu. Tuna timu nzuri, wachezaji wetu wako tayari na bila shaka watapambana kupata matokeo mazuri ugenini," alisema Fadlu

Simba na CS Constantine ni vinara wa kundi A zote zikipata ushindi wa bao 1-0 katika mechi za raundi ya kwanza

Katika ligi za ndani, Simba inashika nafasi ya pili ligi kuu ya NBC huku CS Constantine wakiwa wanaongoza ligi ya kwao Algeria

Ni wazi itakuwa vita ya timu mbili bora zaidi katika kundi A


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post