Taarifa mpya kutoka yanga ni kuhusu Wachezaji wote Majeruhi

 

Kiungo fundi wa Yanga Clatous Chama ataukosa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mashujaa Fc ambao utapigwa kesho Alhamisi katika uwanja wa KMC Complex

Chama alipata majeraha ya kiwiko katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya TP Mazembe ambao ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amethibitisha kuwa Chama atakosekana katika mchezo huo akiuguza jeraha hilo

"Chama alipata jeraha la kiwiko katika mchezo dhidi ya TP Mazembe. Alipoingia tu katika mchezo huo alianguka vibaya na kuumia kiwiko lakini alivumilia akamaliza dakika zote"

"Hivyo yeye atakosekana kutokana na changamoto hiyo inayomkabili," alisema Kamwe

Aidha Kamwe amebainisha kuwa beki Chadrack Boka ameimarika, ana asilimia 50 za kutumika katika mchezo huo kama ilivyo kwa mlinda lango Djigui Diarra ambaye alipata maumivu katika mchezo dhidi ya TP Mazembe na kushinda kumalizia dakika 45 za kipindi cha pili

Aziz Andabwile pia anaendelea kukosekana kama ilivyo kwa beki Ibrahim Bacca anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu akikosa mechi tatu

Hii itakuwa mechi ya mwisho kwa Bacca kukosekana kwani atakuwa amemaliza adhabu yake

Usikose kuitazama mechi SIMBA 🆚 KENGOLD leo na YANGA 🆚 MASHUJAA kesho Live buree kupitia simu yako download App yetu ili kutazama mechi hii pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv mfano Azam two, Sinema zetu na nyingine nyingi

Kudownload  Bonyeza hapa ili kudownload App

Au


App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK kisha uta Install kawaida tu na uendelee kufurahia chanel za Azam na Dstv bureee

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post