Nyota wa Yanga Clatous Chama na Kennedy Musonda wanaendelea kuimarika kutokana na changamoto zinazowakabili pengine nyota hao huenda wakarejea mapema
Chama yuko nje akiuguza jeraha la kiwiko cha mkono ambapo nyota huyo alipewa mapumziko ya siku tano kabla ya kuanza mazoezi mepesi
Musonda pia alipata shida ya kidole cha mguu kupata jeraha ambapo kulingana na taarifa ya kitabibu iliyotolewa na Yanga, nae alihitaji siku tatu za mapumziko kabla ya kuanza mazoezi mepesi ambayo hayataathiri uponaji wa kidonda
Chama na Musonda huenda wakarejea mapema wakati kiungo kiraka Maxi Nzengeli anaweza kuhitaji upasuaji wa goti
Maxi aliumia wakati wa maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabinggwa dhidi ya TP Mazembe ambapo nyota huyo alipewa mapumziko ya hadi siku 14 akiendelea na matibabu ya kawaida na baadae atafanyiwa vipimo zaidi kubaini kama amepona au afanyiwe upasuaji wa goti
Aidha mlinda lango Djigui Diarra anaendelea kutibiwa changamoto ya misuli aliyopata katika mchezo dhidi ya TP Mazembe
Kulingana na taarifa ya Yanga, majeraha ya Diarra yanaweza kuhitaji hadi wiki sita kupona lakini madaktari wanapambana ili kuhakikisha anarejea mapema
Nyota mwingine aliyekuwa majeruhi Aziz Andambwile ameanza mazoezi mepesi na huenda akajiunga na mazoezi ya timu karibuni
Yanga inakabiliwa na mechi muhimu ya marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya TP Mazembe ambayo itapigwa Januari 03 2025 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Madaktari wa Yanga wanapambana kuhakikisha wanapunguza idadi ya majeruhi kabla yha mchezo huo ambao Yanga inahitaji ushindi ili kufufua matumaini ya kutinga robo fainali CAF CL
Usikose kuitazama mechi ya DODOMA JIJI 🆚 YANGA na SIMBA 🆚JKT TANZANIA Live buree kupitia simu yako download App yetu mapema ili kutazama mechi hizi pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv mfano Azam two, Sinema zetu na nyingine nyingi
Kudownload Bonyeza hapa ili kudownload App
Au
App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK kisha uta Install kawaida tu na uendelee kufurahia chanel za Azam na Dstv bureee
Post a Comment