Taarifa Mpya kutoka Yanga leo Jumanne


Usikose kuitazama mechi ya TP MAZEMBE 🆚 YANGA na SIMBA 🆚 CS SFAXIEN  Live buree kupitia simu yako download App yetu ili kutazama mechi hii pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv mfano Azam two, Sinema zetu na nyingine nyingi

Kudownload App Bonyeza hapa



Baada ya kurejea kutoka Algeria jana, kikosi cha Yanga kesho Jumatano kinatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam kuelekea Lubumbashi DR Congo kwa ajili ya mchezo wa raundi ya tatu ligi ya mabingwa dhidi ya TP Mazembe

Jumamosi, Disemba 14 2024 TP Mazembe watakuwa wenyeji wa Yanga katika mchezo muhimu wa kundi A

Yanga imepoteza mechi zote mbili zilizopita, haipaswi kupoteza mchezo huo ili kufufua matumaini ya kufuzu robo fainali

Utakuwa mchezo mgumu kwani hata TP Mazembe ni mechi ambayo watahitaji kushinda ili kuwa na nafasi ya kufuzu robo fainali

Mazembe wanashika nafasi ya tatu kundi A wakiwa na alama moja ambayo waliipata kwa kulazimishwa suluhu ya bila kufungana na MC Alger hapo Lubumbashi

Mechi dhidi ya Yanga itakuwa mechi yao ya pili nyumbani na pengine inaweza kuamua hatma yao katika ligi ya mabingwa msimu huu

Hivyo Wananchi watakwenda Lubumbashi huku wakifahamu wanakwenda kucheza mechi ya 'jasho na damu'

Lakini Yanga ina kumbukumbu nzuri katika dimba la Mazembe kwani mara ya mwisho walipocheza katika uwanja huo msimu wa 2022/23 katika kombe la Shirikisho, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0

Usikose kuitazama mechi hii Live buree kupitia simu yako download App yetu ili kutazama mechi hii pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv mfano Azam two, Sinema zetu na nyingine nyingi

Kudownload  Bonyeza hapa ili kudownload App

Au


App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK kisha uta Install kawaida tu na uendelee kufurahia chanel za Azam na Dstv bureee


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post