Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amesema licha ya kufunguliwa mashtaka ya madai na klabu ya Yanga, ataendelea 'kuwakera' watani zake hao
Akizungumza na wanahabari alfajiri ya leo muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kuelekea Algeria kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya CS Constantine, Ahmed amethibitish kupokea barua kutoka Yanga inayomtaka kuomba radhi na kulipa fidia ya Tsh Bilioni 10 kwa madai ya kuichafua klabu hiyo
"Ni kweli nimepokea barua ya madai kutoka Yanga, lakini sitapenda kuzungumza zaidi kuhusu hilo kwa sababu ni masuala ya kisheria zaidi"
"Lakini niwahakikishie Semaji hatapoa, nitaendelea kuwapelekea moto kama kawaida"
"Kama wadhani watapata ahueni niwaambie tu, barua zao nitaendelea kuzipokea na siachi kuwapelekea moto," alitamba Ahmed
Hivi karibuni Msambazaji wa jezi za klabu ya Simba Sandalan The Only One alimfungulia madai msemaji wa Yanga Ali Kamwe baada ya kutoa kauli zilizolenga kudhoofisha mauzo ya jezi za Simba na kumchafua Sandaland na klabu ya Simba kwa ujumla
Kupitia Wanasheria wake, Sandaland alimtaka Kamwe kuomba radhi na kulipa fidia ya Tsh Bilioni 3
Kitendo cha Yanga kumfungulia madai Ahmed kinatafsiriwa kama 'kujibu mapigo'
Usikose kuitazama mechi ya CS CONSTANTINE 🆚 SIMBA na MC ALGER 🆚 YANGA Live buree kupitia simu yako download App yetu ili kutazama mechi hii pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv mfano Azam two, Sinema zetu na nyingine nyingi
Kudownload Bonyeza hapa ili kudownload App
Au
App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK kisha uta Install kawaida tu na uendelee kufurahia chanel za Azam na Dstv bureee
Post a Comment