Ni kufa au kupona Lubumbashi leo

Kikosi cha Yanga leo Jumamosi saa 10 jioni kwa saa za Tanzania ikiwa ni saa 9 Alasiri huko Lubumbashi kitakuwa dimbani pale TP Mazembe Stadium kumenyana na wenyeji wao TP Mazembe katika mchezo wa raundi ya tatu hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika

Ni mechi muhimu kwa Yanga lakini pia ni mechi muhimu kwa TP Mazembe, hivyo ni sahih kusema ni mechi ya kufa au kupona kwa Yanga

Baada ya kupoteza mechi mbili za kwanza hakuna tena nafasi kwa Yanga kupoteza mchezo ili dhamira ya kutinga robo fainali ibaki hai

Dakika 90 za mchezo wa leo zitaamua kama Yanga bado ifikirie safari yake ya robo fainali au ianze kujipanga kwa ajili ya michuano ya mwakani

Haitakuwa kazi rahisi kupata ushindi mbele ya mabingwa mara tano wa ligi ya mabingwa ambao nao wanaamini leo wanapaswa kushinda baada ya mwanzo mbaya katika hatua ya makundi

TP Mazembe ina alama moja waliyoipata katika mchezo wa kwanza ambao walilazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya MC Alger hapo nyumbani

Leo itakuwa mechi yao ya pili katika uwanja wa nyumbani, Nao wanafahamu kama watakosa ushindi leo pengine safari yao itakuwa imeishia hapo

Ama kwa hakika zitakuwa dakika 90 za kuvuja jasho jingi kwa vijana wa kocha Sead Ramovic, ushindi katika mchezo huo utadhihirisha dhamira ya Yanga kulitaka taji la Afrika

Kila la kheri Wananchi...!

Usikose kuitazama mechi ya TP MAZEMBE 🆚 YANGA Live buree kupitia simu yako download App yetu ili kutazama mechi hii pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv mfano Azam two, Sinema zetu na nyingine nyingi

Kudownload  Bonyeza hapa ili kudownload App

Au


App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK kisha uta Install kawaida tu na uendelee kufurahia chanel za Azam na Dstv bureee


 

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post