Musonda anaamini ushindi unapatikana popote
Mshambuliji wa Yanga Kennedy Musonda amesema hawana hofu yoyote kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya MC Alger ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa July 05, 1962
Musonda amesema wao kama wachezaji wanachofikiria ni kufanya vizuri katika mchezo huo kwaani matokeo ya mechi za nyuma hayawezi kuathiri kile ambacho wanaweza kufanya
Musonda amesema kikosi cha Yanga kina wachezaji wengi ambao wako pamoja kwa muda mrefu na wana uzoefu na michuano ya CAF, hivyo anaamini wataweza kupata matokeo mazuri katika mchezo huo
"Wachezaji wengi wapo hapa kwa misimu kama mitatu, ukitazama historia tumepoteza mechi za mwanzo katika mashindano ya CAF mara mbili, siwezi kusema tumezoea lakini tunafahamu namna tunaweza kukabiliana na hali hii"
"Jambo la muhimu ni kupata matokeo mazuri katika mchezo unaofuata na kuhakikisha tunarudi imara zaidi"
"Hatupaswi kufikiria matokeo ya mechi zilizopita, tunapaswa kujitoa kwa asilimia 100 kwa kuwa ni mchezo wa ugenini"
"Katika hatua hizi hakuna mechi ya nyumbani au ugenini, unatakiwa kujitoa kwa asilimia 100," alisema Musonda
Musonda anatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji ya Yanga katika mchezo huo utakaopigwa saa 4 usiku
Usikose kuitazama mechi hii Live buree kupitia simu yako download App yetu ili kutazama mechi hii pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv mfano Azam two, Sinema zetu na nyingine nyingi
Kudownload Bonyeza hapa ili kudownload App
Au
App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK kisha uta Install kawaida tu na uendelee kufurahia chanel za Azam na Dstv bureee
Post a Comment