MC Alger vs Yanga kinapigwa hapa
Usikose kuitazama mechi ya CS CONSTANTINE 🆚 SIMBA na MC ALGER 🆚 YANGA Live buree kupitia simu yako download App yetu ili kutazama mechi hii pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv mfano Azam two, Sinema zetu na nyingine nyingi
Kudownload App Bonyeza Hapa
Leo Yanga inatarajiwa kutua Algiers yalipo Makao Makuu ya Algeria tayari kwa mchezo wa pili wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya MC Alger
Mchezo huo utapigwa Jumamosi, Disemba 07 katika uwanja wa Julai 05, 1962 saa 1 usiku
Yanga inarudi katika uwanja huu mwaka mmoja baada ya mchezo wao wa fainali ya kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger uliomlizika kwa Wananchi kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa Djuma Shaban dakika ya 7 baada ya Kennedy Musonda kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari
Ni hapa hapa Yanga ilicheza mechi ngumu sana iliyogubikwa na kila aina ya matukio ya kustaajabisha katika soka kwani yalipigwa hadi mabomu ya machozi!
Wakati huu wanarudi kucheza dhidi ya MC Alger timu yenye upinzani wa jadi na USM Alger katika mchezo mwingine ambao Yanga inahitaji kushinda
Lakini wakati huu mambo yatakuwa tofauti kwani zile vurugu ambazo Yanga walifanyiwa mwaka jana hazitarajiwi kuwepo
Klabu ya MC Alger imefungiwa kuingiza mashabiki katika mechi zao mbili za nyumbani kufuatia vurugu za mashabiki wao katika mchezo wa kuwania kutinga hatua ya makundi CAF CL dhidi ya US Monastir
Yanga itakuwa timu ya kwanza kucheza na MC Alger bila mashabiki ikiwa sehemu ya kutekeleza kifungo hicho
MC Alger walikata rufaa lakini CAF ilishikilia msimamo huku pia wakigomea maombi ya klabu hiyo kubadili uwanja
Bila shaka kocha Sead Ramovic na vijana wake watakuwa na nafasi ya kufanya vizuri katika mchezo huu ambao hautakuwa na presha kutoka kwa mashabiki
Post a Comment