Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo ambapo vinara wa ligi hiyo Simba watashuka uwanja wa KMC Complex kuikabili JKT Tanzania katika mchezo utakaopigwa saa 10 jioni
Baada ya ushindi mnono wa mabao 5 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo uliopita, Simba imepania kuendeleza ubabe wake leo mbele ya maafande wa JKT
Hautakuwa mchezo mwepesi kwani JKT Tanzania ni miongoni mwa timu ngumu kufungika katika msimu huu
Wakiwa wamecheza mechi 14, JKT Tanzania wamepoteza mechi 3, wakishinda 4 na kutoka sare mechi 7
Hata hivyo wanakutana na Simba yenye rekodi bora zaidi msimu huu, ikishinda mechi 11, sare mchezo mmoja na kupoteza mchezo mmoja
Kocha Msaidizi wa Simba Selemani Matola amesema wanatambua ushindani ambao watakutana nao leo kutoka kwa JKT lakini malengo ya kushinda mchezo huo yako palepale
Itakuwa mechi ya kwanza kwa nahodha wa zamani wa Simba John Bocco kucheza dhidi ya waajiri wake wa zamani, Simba
Ushindi kwa Simba utawahakikishia Wekundu hao wa Msimbazi kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi kabla ya mchezo wa kuhitimisha duru ya kwanza dhidi ya Singida Black Stars utkaopigwa uwanja wa CCM Liti Disemba 28
Usikose kuitazama mechi ya DODOMA JIJI 🆚 YANGA na SIMBA 🆚JKT TANZANIA Live buree kupitia simu yako download App yetu mapema ili kutazama mechi hizi pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv mfano Azam two, Sinema zetu na nyingine nyingi
Kudownload Bonyeza hapa ili kudownload App
Au
App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK kisha uta Install kawaida tu na uendelee kufurahia chanel za Azam na Dstv bureee
Post a Comment