Kuna usajili unasubiri kutangazwa - Kamwe

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema bado hawajafunga hesabu za usajili wa dirisha dogo na wakati wowote watatambulisha usajili wa mchezaji mwingine

Baada ya kukamilisha usajili wa mlinzi wa kulia Israel Mwenda, kumekuwa na ukimya huku zikiwa zimesalia wiki mbili kabla ya dirisha kufungwa

"Katika siku hizi mbili tutakamilisha moja ya sajili kubwa katika dirisha hili. Imekuwa si rahisi kupata wachezaji bora katika dirisha hili kwa sababu wengi bado wana mikataba na timu zao haziko tayari kuwaachia katikati ya msimu"

"Baada ya mvutano wa hapa na pale, hatimaye Yanga imeweza kukamilisha usajili huo na tutauweka hadharani muda wowote"

"Wako pia wachezaji wengine ambao uongozi unaendelea na mazungumzo nao kama tutafikia makubaliano basi nao watasajiliwa"

"Usajili huu unafanyika kwa kuzingatia mapendekezo ya benchi la ufundi kupitia ripoti ambayo iliwasilishwa ofisi ya Mtendaji Mkuu," alisema Kamwe

Baada ya kuachana na Jean Balake, Yanga inatarajiwa kumtangaza mshambuliaji anayechukua nafasi yake huku pia kukiwa na taarifa ya kuongezwa kwa beki mwingine wa kati

Wachezaji wanaosajiliwa pia wanaweza kutumika katika mechi za ligi ya mabingwa kama wtasajiliwa Kimataifa pale dirisha la CAF litakapofunguliwa Januari 01, 2025

Usikose kuitazama mechi ya YANGA 🆚 TP MAZEMBE na CS SFAXIEN 🆚 SIMBA LIVE bure kupitia simu yako download App yetu mapema inayorusha mechi zote live bure pia ukiwa na App yetu utaweza kutazama chanel zote za Azam Tv na DSTV live bure mfano Azam sport 1, Azam Two, Sinema zetu na nyingine nyingi

Kudownload  Bonyeza hapa ili kudownload App

Au


App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK kisha uta Install kawaida tu na uendelee kufurahia chanel za Azam na Dstv bureee


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post