Kisa Simba, CS Constantine yapandisha viingilio

Kisa Simba, CS Constantine yapandisha viingilio

Usikose kuitazama mechi ya CS CONSTANTINE 🆚 SIMBA na MC ALGER 🆚 YANGA Live buree kupitia simu yako download App yetu ili kutazama mechi hii pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv mfano Azam two, Sinema zetu na nyingine nyingi Kudownload App hii bonyeza Hapa


Kikosi cha Simba tayari kimewasili Algeria kwa pambano la pili la Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya CS Constastine, huku wenyeji wakiweka kiingilio cha juu ya Dinar 6000 (zaidi ya Sh 117,000) na kima cha chini cha kiingilio kikiwa ni Dinar 1000, ambayo ni kama Sh 19,000 za Kitanzania.

Wenyeji hao tayari wamanza kuunza tiketi kwa njia ya kisasa wa kidigitali ya mchezo huo utakaopigwa Jumapili. Hii ni sawa na mfumo unaotumika sasa nchini Tanzania katika michezo ya Ligi Kuu Bara na Kimataifa.

Kwa mujibu wa ripoti, CS Constantine tiketi hizo zinauzwa kupitia Tadkirati, jukwaa la mtandao ambalo linawawezesha mashabiki kununua tiketi kwa urahisi na usalama. Tiketi za mchezo huo zitauzwa kwa viwango tofauti, na kima cha chini kikiwa Dinar 1000 (zaidi ya sh. 19,000), huku tiketi za Dinar 6000 (zaidi ya sh. 117,000) zikiwa za viti vya mbele kabisa.

Mashabiki watakaotaka kushuhudia dakika 90 za mchezo huo katika uwanja maarufu wa Mohamed Hamlaoui wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 40,000, watatakiwa kutumia jukwaa la Tadkirati kununua tiketi zao. Mfumo huu umeanzishwa kama njia ya kuhakikisha usalama na udhibiti wa idadi ya mashabiki watakaoingia uwanjani.

Tadkirati, ambayo inatoa nafasi kwa kila mpenzi wa soka kuingiza majina yao pamoja na majina ya wamiliki wa tiketi, imewekwa ili kuhakikisha kwamba tiketi ni za mtu mmoja kwa mmoja. Hii ni hatua madhubuti ya kupunguza ulanguzi na kudhibiti udanganyifu katika ununuzi wa tiketi.

Kwa kuongeza, uongozi wa CS Constantine umeonya kwamba mashabiki wote watakaohudhuria mchezo huo watatakiwa kuonyesha kitambulisho cha kitaifa (NIM) ili kuthibitisha utambulisho wao kabla ya kuingia uwanjani.

Hii ni hatua ya kuhakikisha kwamba hakuna mtu atakayekosa kuingia au kupata usumbufu katika uwanja.

Vilevile, mashabiki wa Simba na wale kutoka maeneo mengine ya jirani, wanatakiwa pia kuonyesha vitambulisho vyao ili kuthibitisha utambulisho wao.

Simba itavaana na CS Constantine ikiwa imetoka kushinda nyumbani bao 1-0 dhidi ya Bravos do Maquis ya Angola, huku wenyeji wao wakipata ushindi kama huo ikiwa ugenini dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia.

Mwanaspoti

Usikose kuitazama mechi hii Live buree kupitia simu yako download App yetu ili kutazama mechi hii pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv mfano Azam two, Sinema zetu na nyingine nyingi

Kudownload  Bonyeza hapa ili kudownload App

Au


App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK kisha uta Install kawaida tu na uendelee kufurahia chanel za Azam na Dstv bureee

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post