KIMENUKA: Yanga kumburuza mahakamani Ahmed Ali

 Klabu ya Yanga imemtaka Meneja habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally kutoka hadharani na kuomba radhi kwa matamshi ya kuichafua klabu ya Yanga

Aidha Yanga imemtaka Ahmed kulipa fidia ya Tsh Bilioni 10 kutokana na kauli aliyotoa hivi karibuni

Katika moja ya mahojiano aliyofanya, Ahmed alisikika akitoa kauli hii;

 "Pacome amemaliza mkataba tukiona anafaa tutahangaika nae, Pacome amemaliza mkataba ndani ya Yanga na hana mpango wa kuongeza"

"Mtanyoa ndevu mwaka huu hana mpango wa kuongeza amechoka kuchomwa sindano kila siku kama anazuia mimba"

"Tunaangalia kiwango chake kama kitaturidhisha tutahangaika nae lakini kama ataendelea na mwenendo wake anaoendelea nao tutawaachia kama tulivyowaachia Chama na tunataja majina Live hakuna kutumia code" 

Taarifa ya madai ya Yanga imeeleza kuwa kauli hiyo ni ya upotoshaji na imejaa dharau kwa klabu yao, hivyo imeharibu mahusiano yao na wadau wa kibiashara na wadhamini

Yanga wamemtaka Ahmed afanye yafuatayo ndani ya siku tano (5);

  1. Kuomba radhi kwa njia sawa na aliyotumia kutoa kauli yake
  2. Kufidia malipo ya Tsh Bilioni 10 (10,000,000,000)

Yanga imetahadharisha kuwa kama maagizo hayatafanyiwa kazi watafuata hatua za kisheria zaidi

Usikose kuitazama mechi ya CS CONSTANTINE 🆚 SIMBA na MC ALGER 🆚 YANGA Live buree kupitia simu yako download App yetu ili kutazama mechi hii pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv mfano Azam two, Sinema zetu na nyingine nyingi

Kudownload  Bonyeza hapa ili kudownload App

Au


App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK kisha uta Install kawaida tu na uendelee kufurahia chanel za Azam na Dstv bureee

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post