Baada ya kuishushia Dodoma Jiji kipigo cha mabao 4-0, kikosi cha Yanga kilirejea jijini Dar es salaam jana kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya kuhitimisha mwaka 2024
Itakuwa Jumapili, Disemba 29 katika uwanja wa KMC Complex Yanga itamenyana na Fountain Gate, mchezo utakaopigwa saa 10 jioni
Hii ndio mechi ya mwisho ya ligi kuu kwa Yanga 2024. Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewataka Wananchi wa jijini Dar es salaam kuhakikisha wanakata tiketi mapema
Pia utakuwa ni mchezo wa kukamilisha raundi ya 15 kwa Yanga, alamu tatu zinaweza kuwarudisha Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi hasa endapo Simba itakosa ushindi dhidi ya Singida Black Stars
Chini ya kocha Sead Ramovic Yanga imekuwa ikitembeza vipigo katika ligi kuu ya NBC, ikifunga mabao 13 na kuruhusu mabao 2 katika mechi 4 huku ikikusanya alama 12
Ni wazi Fountain Gate watakuwa na kazi kubwa Jumapili, 'Gusa achia twende kwao' inaweza kuwasababishia maafa
Fountain Gate wameruhusu mabao 27 katika mechi 15 walizocheza mpaka sasa. Wanakutana na Yanga ambayo washmbuliaji wake Prince Dube na Clement Mzize wako moto katika kuzifumania nyavu
Usikose kuitazama mechi ya SINGIDA BS 🆚 SIMBA na YANGA 🆚 SINGIDA FG LIVE bure kupitia simu yako download App yetu mapema inayorusha mechi zote live bure pia ukiwa na App yetu utaweza kutazama chanel zote za Azam Tv na DSTV live bure mfano Azam sport 1, Azam Two, Sinema zetu na nyingine nyingi
Kudownload Bonyeza hapa ili kudownload App
Au
App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK kisha uta Install kawaida tu na uendelee kufurahia chanel za Azam na Dstv bureee
Post a Comment