Ahmed awaalika Wanasimba KMC Complex kushuhudia shoo za Mpanzu

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amewaalika mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi dimba la KMC Complex kushuhudia shoo za 'winga tareza' Elie Mpanzu

Leo Simba itakuwa mwenyeji wa JKT Tanzania katika mchezo utakaopigwa saa 10 jioni

Ahmed amesema mashabiki wa Simba walikuwa na shauku kubwa ya kumshuhudia winga huyo katika mchezo dhidi ya KenGold lakini haikuwezekana baada ya vibali vyake kutopatikana kwa wakati

"Mashabiki wa Simba hapa Dar walitamani sana kuwa wa kwanza kushuhudia shoo za Elie Mpanzu lakini bahati hiyo wakaipata Wanasimba wa Bukoba"

"Sasa leo nawaalika waje kwa wingi KMC Complex kushuhudia shoo za Mpanzu aka Father Christmas," alitamba Ahmed

Katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 5-2, Mpanzu alicheza kwa takribani dakika 57

Kocha Fadlu Davids leo anatarajiwa kumuanzia tena katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania ikiwa ni mechi yake ya kwanza nyumbani

Usikose kuitazama mechi ya DODOMA JIJI 🆚 YANGA na SIMBA 🆚JKT TANZANIA Live buree kupitia simu yako download App yetu mapema ili kutazama mechi hizi pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv mfano Azam two, Sinema zetu na nyingine nyingi

Kudownload  Bonyeza hapa ili kudownload App

Au


App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK kisha uta Install kawaida tu na uendelee kufurahia chanel za Azam na Dstv bureee

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post