Licha ya tetesi kuzagaa kuhusu mustakabali wake, mpaka sasa Miguel Gamondi bado ndiye kocha wa Yanga akiweka sawa mipango ya mandalizi ya kikosi chake kuelekea mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal
Novemba 27 Yanga itakuwa mwenyeji wa Al Hilal dimba la Benjamin Mkapa katika mchezo ambao utakuwa kama kisasi kwa Yanga
Sare ya bao 1-1 uwanja wa Benjamin Mkapa Oktoba 08 na kipigo cha bao 1-0 katika mchezo wa pili uliopigwa Khartoum, uliishuhudia Yanga ikitupwa nje ya michuano ya ligi ya mabingwa na Al Hilal mwaka 2022 na Wananchi kuangukia katika kombe la Shirikisho ambalo walikwenda kucheza fainali
Ni kumbukumbu hii ambayo inapelekea mechi mbili dhidi ya Al Hilal katika makundi kuwa umuhimu wa kipekee kwa Yanga
Yanga inazihitaji alama zote sita dhidi ya Al Hilal ambao mechi zao za nyumbani watachezea Libya
Habari njema kwa Yanga ni kuwa baada ya kucheza mechi mfululizo, angalau wachezaji watapata muda wa kutosha kujiandaa na mchezo huo licha ya kuwa bado wachezaji 10 watakosekana kutokana na majukumu ya timu za Taifa
Djiguo Diarra (Mali), Khalid Aucho (Uganda), Prince Dube (Zimbabwe), Duke Abuya (Kenya), Kennedy Musonda na Clatous Chama (Zambia), wameungana na Ibrahim Bacca, Dickson Job, Mudathir Yahya na Clement Mzize walioitwa timu ya Taifa ya Tanzania
Awali ratiba ilikuwa ikionyesha kabla ya kuchuana na Al Hilal, Yanga ilipaswa kucheza mechi ya ligi kuu dhidi ya Fountain Gate hata hivyo mchezo huo umesogezwa mbele ili kuipa nafasi Yahga kujiandaa na mchezo huo wa ligi ya mabingwa
Wachezaji waliokwenye majukumu ya timu za Taifa pia watapata muda wa kuiwahi mechi hiyo kwani kalenda ya FIFA itahitimishwa Novemba 19 wakati mchezo ukitarajiwa kupigwa Novemba 27
Usikose kuitazama mechi hii ya kibabe live kupitia simu yako download app yetu itakayo rusha mechi hii live buree.
Post a Comment