Kikosi cha Yanga jana mchana kiliwasili mkoani Lindi kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Namungo unaotarajiwa kuchezwa kesho, Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa
Kuelekea mchezo huo, Kocha Mkuu wa Yanga, Sead Ramovic, ameahidi kurejea kwa kasi ligi kuu baada ya kurekebisha mapungufu aliyoyaona kwenye mchezo uliopita wa Ligi ya Mabingwa Afrika, dhidi ya Al Hilal Omdurman ya Sudan uliochezwa Jumanne iliyopita, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam
Yanga imewasili Lindi ikiwa na kikosi kamili tayari kuwafuta machozi mashabiki wake ambao wamekosa furaha baada ya kupata vichapo vitatu mfululizo katika mechi tatu zilizopita
Akizungumza jana muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kuifuata Namungo, Ramovic alisema kwa sasa wamefanyia kazi mapungufu aliyoyaona kwenye mchezo uliopita dhidi ya Al Hilal na sasa wapo tayari kwa mchezo huo wa kesho
"Kama nilivyosema suala ya utimamu huwezi kulitatua kwa muda mfupi, lakini tumeanza kulifanyia kazi, na nadhani linaweza kukaa sawa baada ya muda, kwa sasa nataka turejee kwenye michezo ya Ligi kwa kasi" alisema Ramovic
Mchezo dhidi ya Namungo, utakuwa wa kwanza kwa kocha huyo kuiongoza Yanga kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu baada ya kuondoka kwa Miguel Gamondi ambaye aliipa ubingwa msimu uliopita na msimu huu aliiongoza kwenye michezo 10, ikishinda minane na kupoteza miwili
Mara baada ya mechi dhidi ya Al Hilal, Ramovic alibainisha kuwa wachezaji wake walionekana hawana utimamu wa mwili pamoja na pumzi ya kucheza kwa dakika 90 kwa nguvu ile ile, hivyo kuahidi kulifanyia kazi suala hilo
Usikose kuzitazama live mechi zote kupitia simu yako download app yetu itakayo kuwezesha kuzitzama mechi zote live buree pia ukiwa na App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv mfano Azam sport 1,2,3, Azam Two,Sinema Zetu na nyingine nyingi download app yetu mapema kudownload app yetu bonyeza neno download hapa chini👇🏻👇🏻 App bado hatujaiweka playstore hivo bonyeza kitufe cha download Anyway
Kudownload App Bonyeza Hapa kudownload
Post a Comment