Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids, amewapa kazi mastraika wake wawili, Leonel Ateba na Steven Mukwala, kuwamaliza Waangola, Bravo do Maquis, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, unaotarajiwa kuchezwa, Jumatano katika Uwanja wa Benjamin Mkapa
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, kocha huyo raia wa Afrika Kusini, alisema kwa jinsi alivyowaangalia wapinzani wao, anadhani mastraika wake wana uwezo wa kuimaliza mechi hiyo kwa jinsi wanavyocheza
"Malengo ni kupata ushindi nyumbani, ikiwezekana mkubwa tu, kwa kutumia nafasi tutakazotengeneza zitumiwe kwa usahihi na mastraika wetu ambao tumewapa kazi hiyo tu, kiufundi tayari tumeshawaangalia wapinzani wetu kwenye baadhi ya mechi, hasa ya Ijumaa, Novemba 22, waliyocheza dhidi ya Academica de Lobito kwenye Ligi Kuu nchini Angola," alisema
Hii itakuwa mara ya pili kwa Bravos kucheza nchini katika kombe la Shirikisho msimu huu
Katika hatua ya mtoano walikuja kucheza dhidi ya Coastal Union katika mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex na kumalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana
Bravos walisonga mbele hatua iliyofuata baada ya kushinda mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Angola
Usikose kuitazama mechi ya YANGA vs AL HILAL na SIMBA vs BRAVO download app yetu mapema ili usipitwe Bonyeza Hapa kudownload
Post a Comment