Fataki zapigwa marufuku leo uwanja wa Benjamini Mkapa

 

Uongozi wa klabu ya Yanga umewataka mashabiki watakaojitokeza uwanja wa Benjamin Mkapa leo katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal kutofanya vurugu ili kuepuka adhabu ya Shirikisho la soka barani Afrika (CAF)

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema mashabiki hawapaswi kuwasha fataki, moto au kufanya vurugu za aina yoyote

"Niwaombe mashabiki wote mtakaokuja uwanjani, tuendeleze utamaduni wetu wa amani na utulivu, tushangilie timu yetu kistaarabu bila ya vurugu wala kuwasha moto na kupiga fataki"

"Baadhi ya timu zimefungiwa kuingiza mashabiki katika mechi zao kutokana na matukio ya aina hiyo. Hivyo tunapaswa kuepuka vurugu za aina yoyote ili tuhakikishe mechi zetu zote tutakazocheza nyumbani mashabiki wanaruhusiwa," alisema Kamwe

MC Alger ya Algeria ni miongoni mwa klabu ambazo zimefungiwa kuingiza mashabiki katika mechi zao kutokana na matukio ya vurugu

Baada ya mchezo dhidi ya Al Hilal, mchezo utakaofuata Yanga itachuana na MC Alger huko Algeria Disemba 07 na kutokana na kifungo hicho ya MC Alger, hakutakuwa na mashabiki

Usikose kuitazama mechi ya YANGA vs AL HILAL Live (mubashara) buree kupitia simu yako download app itakayo rusha mechi hii live kabisa bure ili uweze kuitazama mechi hii.

Pia ukiwa na App hii utaweza kutazama chanel za Azam tv kama Azam sport 1,2,3 Azam Two, Sinema zetu, Wasafi, Crown Tv, Zamaradi Tv na nyingine nyingi

Kudownload App hii bonyeza 👉🏻HAPA

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post