Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetangaza viwango vipya vya adhabu kwa timu zote zinazoshiriki Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho zitakazoshindwa kuzingatia kikamilifu kanuni
Yanga na Simba zinaiwakilisha Tanzania katika michuano hiyo ambayo hatua ya makundi itaanza kutimua vumbi mwishoni mwa mwezi huu
Kwa mujibu wa kanuni hizo, kila timu inapaswa kutumia mipira rasmi ya CAF ambapo kama timu itatumia mpira usio rasmi wakati wa mechi itapigwa faini ya USD 40,000 kutoka USD USD 30,000
Lakini pia kutumia nembo isiyo rasmi faini ya hadi USD 10,000 kutoka USD 2,000. Kutoheshimu rangi za vifaa vinavyowasilishwa na CAF faini yake hadi USD 40,000 kutoka USD 10,000.
Kutoonekana kwa majina ya wachezaji kwenye jezi faini yake ni hadi USD 20,000 kutoka USD 5,000. Benchi la ufundi ambalo litatumia mavazi yenye chapa ambayo haijaidhinishwa faini yake ni hadi USD 60,000.
Huu hapa mkeka wa leo bure👉🏻 B53248 kama bado hujajisajili na Galsport Bonyeza HAPA kujisajili kisha weka Dau na ushinde ( Ushindi kwetu ni kila siku )
Post a Comment