Afisa Habari wa Bodi ya Ligi Karim Boimanda amesema uamuzi wa Yanga kubadili uwanja kutoka Azam Complex kuhamia KMC Complex uko sawa kwa mujibu wa kanuni
Boimanda amesema TPLB imepokea ombi la Yanga na kinachosubiriwa ni uamuzi wa Bodi
Boimanda ameitaja Kanuni ya 9(4) kuwa inawapa haki Yanga na timu nyingine ambazo hazina uwanja wake inaoumiliki kuhama kama tu hawakuwa na makubaliano na wamiliki
"Novemba 10 Bodi ilipokea ombi la Yanga kuhusu kubadili uwanja kutoka Azam Complex walipokuwa wakicheza awali na kuomba kuhamia KMC Complex. Ombi lao linaangukia katika kanuni ya 9(4)"
"Kanuni hiyo inawapa Yanga na timu nyingine ambazo hazina uwanja wake inaoumiliki haki ya kuhama kama hawana makubaliano na wamiliki"
"Kwa mujibu wa kanuni hiyo, timu inaruhusiwa kutafuta uwanja ndani ya mkoa husika au mkoa wa jirani, sharti kuu ni lazima uwanja huo ukidhi vigezo"
"Kabla ya kufanya maamuzi jambo la kwanza kuangaliwa ni kanuni na kama nilivyosema ombi lao linaangukia kanuni ya 9(4)"
"Pia yatazingatiwa mambo mengine kama ratiba, Yanga imetoka katika uwanja ambao mechi zilikuwa zinachezwa jioni na usiku na wameomba kuhamia katika uwanja ambao mechi zinachezwa jioni tu"
"Hivyo niseme tu mpaka sasa Bodi bado haijajibu maombi hayo kutokana na taratibu za kiuendeshaji ambapo pale zitakapokamilika wataarifiwa," alisema Boimanda
Usikose kuitazama mechi hii ya kibabe leo kati ya YANGA PRINCESS vs SIMBA QUEENS Live bure kupitia simu yako download App yetu kutazama mechi hii.
Mechi itapigwa majira ya saa 10:00 jioni kwenye uwanja wa Kmc Complex.
Pia ukiwa na App yetu Utaweza kutazama chanel kama:
Post a Comment