Baada ya hapo jana Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha kusema endapo timu ya Tabora United ikiifunga Simba kwenye mchezo wa Ligi kuu bara utakaochezwa Desemba 28 mwaka huu basi atawazawadia motisha ya Tsh 50 Milioni, msemaji wa Simba Ahmed Ali amesema Simba sio timu ya kuwekewa ahadi
Mkuu huyo wa mkoa aliiahidi Tabora Unitd kitita cha Tsh Milioni 20 kama ingeifunga Yanga, jana alikabidhi fedha hizo baada ya ushindi wa mabao 3-1 ambao Tabora United waliupata dhidi ya Yanga
Ahmed ametamba kuwa Tabora United wasitarajie kupata fedha hizo kwani Simba sio timu ya kuwekea ahadi
"Mnajisumbua tu Simba sio timu ya kuiwekea ahadi," aliandika Ahmed katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Tabora United ilikuwa timu ya kwanza kuonja kichapo cha Simba msimu huu katika mechi ya ufunguzi wa ligi kuu Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa KMC Complex
Mchezo wa duru ya pili utapigwa Disemba 28 uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora
Usikose kuitazama mechi ya kibabe kati ya SIMBA vs PAMBA na YANGA vs AL HILAL Live bure kupitia simu yako download App yetu kutazama mechi hii.
Pia ukiwa na App yetu Utaweza kutazama chanel kama:
Post a Comment