Ahadi ya kocha mkuu mpya wa Yanga Ramovic kwa Wananchi

 Kocha Mkuu  wa Yanga, Sead Ramovic raia wa Ujerumani, ameonesha furaha kubwa kupata nafasi ya kuifundisha timu kubwa kama hiyo, huku akisema anaifahamu sana Simba na kumtaja kocha wa timu hiyo, Fadlu Davids, kuwa ni rafiki yake

Akizungumza kwa mara ya kwanza baada ya kutangazwa kuwa Kocha Mkuu, akichukua nafasi ya Miguel Gamondi, Sead aliyetokea Klabu ya TS Galaxy ya Afrika Kusini, aliwataka wanachama, mashabiki, wapenzi, viongozi na wao kama makocha kuungana kwa pamoja ili kufikia malengo

"Ni heshima kubwa sana kuwa hapa kuifundisha hii timu, ni klabu kubwa sana yenye wachezaji wenye vipaji vikubwa, na ni fahari kuwaongoza na kuendeleza mafanikio ya klabu hii yenye mataji mengi, na nia yangu ni kufanya kila ninachoweza ili kulinda yaliyopo na kuleta mengine mapya," alisema

Ramovic alisema alikiona kikosi hicho nchini Afrika Kusini kilipokwenda kucheza michezo ya kirafiki ya kimataifa kabla ya kuanza msimu mpya

"Nilikiona kikosi cha Yanga kilipocheza na FC Augsburg ya Ujerumani, wakacheza na sisi pia TS Galaxy, niliona kuwa ni timu iliyokuwa na wachezaji wenye vipaji sana, lakini pia naona fahari sana kuifundisha timu hii yenye mashabiki wengi sana nchini, siwezi kusema nalifahamu sana soka la Tanzania, lakini najua kuwa Yanga ndiyo timu bora kwa sasa hapa nchini," alisema

Pamoja na hayo, alisema anaifahamu sana timu ya Simba, huku pia akisema kocha wa sasa wa timu hiyo, Fadlu ni rafiki yake sana

"Naifahamu pia Simba kwa sababu kocha wao, Fadlu ni rafiki yangu, alikuwa mwalimu wa Orlando Pirates wakati huo wote tukiwa Afrika Kusini," alisema

Kocha huyo ataanza mtihani wake wa kwanza Novemba 26, mwaka huu, atakapokiongoza kikosi cha Yanga kucheza mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal Omdurman ya Sudan, utakaochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam

Gamondi aliifikisha timu hiyo hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita na kutolewa kwa mbinde na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwa mikwaju ya penalti 3-2, Aprili 5, mwaka huu, huko Sauzi

Hatua hiyo ya 'matuta' ilifikiwa baada ya suluhu mbili, ya kwanza ikipatikana kwenye mchezo wa awali uliochezwa, Machi 30, mwaka huu, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam

Kocha huyo pia ana kazi nyingine ya kuulinda ubingwa aliouchukua Gamondi msimu uliopita, ambaye ametemwa akiwa kwenye nafasi ya pili ya msimamo msimu huu akiwa ameiongoza michezo 10, kushinda minane na kupoteza miwili dhidi ya Azam FC na Tabora United, ambayo inadhaniwa kwa kiasi kikubwa kuwa chanzo cha kufutwa kazi kwa Muargentina huyo

IPP Media

Usikose kuitazama mechi hii Live (mubashara) buree kupitia simu yako download app itakayo rusha mechi hii live kabisa bure uweze kuitazama mechi hii.

Pia ukiwa na App hii utaweza kutazama chanel za Azam tv kama Azam sport 1,2,3 Azam Two, Sinema zetu, Wasafi, Crown Tv, Zamaradi Tv na nyingine nyingi

Kudownload App hii bonyeza 👉🏻HAPA

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post