Yanga iko tayari kukabiliana na vigogo CAF CL
Droo ya hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika inafanyika leo huko Misri saa 8 mchana
kabla ya droo ya mabingwa, itatangulia droo ya kombe la Shirikisho itakayofanyika saa 7 mchana
Baada ya mafanikio ya msimu uliopita kucheza robo fainali na kuondolewa katika hatua hiyo kwa matuta dhidi ya Mamelodi Sundowns ambao walinufaika na makosa ya mwamuzi aliyekataa bao halali la Yanga katika muda wa kawaida, Yanga iko tayari kufanya zaidi ya msimu uliopita
Yanga itakuwa poti ya pili pamoja na CRB (Algeria), Raja CA (Morocco) na Pyramids FC (Egypt)
Katika kundi lake Yanga itapangwa na timu moja kutoka kila pot yaani pot 1, pot 3 na pot 4
Pot 1 zipo Al Ahly SC (Egypt), Esperance Sportive de Tunis (Tunisia), Mamelodi Sundowns (South Africa) na TP Mazembe (DR Congo)
Pot 3 zipo Al Hilal (Sudan), Orlando Pirates (South Africa), GD Sagrada Esperanca (Angola) na AS FAR (Morocco)
Pot 4 zipo MC Alger (Algeria), AS Maniema Union (DR Congo), Djoliba de Bamako (Mali) na Stade d'Abidjan (Cote d'Ivoire)
Yanga ni miongoni mwa timu zinazopewa nafasi ya kufanya vizuri zaidi katika michuano ya msimu huu kutokana na kile walichofanya msimu uliopita
Timu kama Mamelodi Sundowns ambayo msimu uliopita ilionja radha ya soka la Yanga ni wazi hawatatamani kukutana na Yanga kwa mara nyingine wakati Wananchi wanawatamani ili kumalizana nao
Msimu uliopita Yanga ilikuwa kundi moja na Al Ahly, ikitokea tena wakati huu wakawa kundi moja, itakuwa nafasi kwa wananchi kulipa kisasi cha kupoteza mchezo wa pili ugenini dhidi ya mabingwa hao watetezi
Esperance ni timu pekee kutoka pot 1 ambayo kama itapangwa na Yanga itakuwa mara ya kwanza kwa timu hizo kukutana
TP Mazembe ilikuwa na Yanga katika kombe la Shirikisho 2022/23 'ikipasuka' mechi zote mbili dhidi ya mabingwa hao wa Tanzania Bara
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
Post a Comment