Ratiba ya Mechi za Simba mwezi huu wa kumi - EDUSPORTSTZ

Latest

Ratiba ya Mechi za Simba mwezi huu wa kumi

 

Jana Bodi ya Ligi iliweka hadharani ratiba mpya ya mechi za Ligi kuu baada ya kufanyika maboresho kwenye baadhi ya mechi

Katika kipindi cha siku 10 Simba itacheza mechi nne za ligi ikianza na mchezo dhidi ya Yanga siku ya Jumamosi, Oktoba 19 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Baada ya mchezo huo, Simba itasafiri mkoani Mbeya kuikabili, Tanzania Prisons katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Sokoine, Oktoba 22

Ikitoka Mbeya, Simba itarudi Dar kuikabili Namungo Fc katika mchezo utakaopigwa Oktoba 25 katika uwanja wa KMC

Oktoba 29 Simba itarudi tena KMC Complex kuikabili JKT Tanzania

Mnyama ataanza mwezi Novemba mkoani Kigoma kwa mchezo dhidi ya Mashujaa Fc utakaopigwa Novemba mosi na kisha kurejea Dar kuikabili KMC Novemba 05

KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA


PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE  HAPA



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz