Mnao iponda yanga mnapata wapi ujasiri, Ubora wa timu unapimwa kwa mafanikio yake
Usikose kuitazama mechi ya kibabe kati ya SINGIDA BS vs YANGA leo live kupitia simu yako download app yetu itakayo rusha mechi hii live buree pia ukiwa na app yetu utaweza kutazama chanel za AZAM TV mfano AZAM TWO, SINEMA ZETU, AZAM SPORT 1 na nyingine nyingi pia utaweza kutazama chanel za DSTV Bure na Muvi zilizo tasfiriwa kwa kiswahili, Kudownload App yetu bonyeza 👉🏻HAPA
Ubora wa timu unapimwa kwa mafanikio yake
Ukisikiliza uchambuzi katika redio mbalimbali nchini kila baada ya mechi ya Yanga, utasikia hii kauli ya kuwa Yanga imeshuka ubora wake kulinganisha na msimu uliopita
Wachambuzi wanaotoa kauli hii nafikiri ni maoni yao binafsi na sio kwa mujibu wa takwimu. Kwani wanaposema Yanga imeshuka ubora walipaswa kutonyesha ni kwa namna gani
Takwimu za Yanga msimu huu zinapingana na maoni yao. Bahati mbaya ni kuwa wakati mwingine maoni hayo hutafsiriw tofauti na baadhi ya mashabiki pasipo kuzingatia uhalisia
Kwa mujibu wa takwimu, Yanga imeanza vyema zaidi msimu huu pengine zaidi kuliko ilivyofanya katika misimu ya hivi karibuni
Hii timu inayosemwa imepungua ubora, imeshinda mechi saba za ligi bila kuruhusu bao! Ndio mabingwa wa Ngao ya Jamii waliyoichukua mbele ya Azam Fc, Simba na Coastal Union
Wametinga hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa kibabe wakifunga mabao 17 na kuruhusu bao moja tu
Ukichukua kuanzia msimu uliopita, Yanga imecheza mechi 17 za ligi bila ya kupoteza, ikicheza mechi 45 uwanja wa nyumbani bila kupoteza
Ukichukua mechi za mashindano yote tangu wakati wa pre-season, Yanga imepoteza mchezo mmoja tu dhidi ya Augsburg inayocheza Bundesliga Ujerumani
Imefunga bao katika kila mechi iliyocheza tangu Julai 20 2024! Tunazungumzia zaidi ya mechi 18 za mashindano na kirafiki!
Kuna wale waliokariri kuwa timu bora haipaswi kushinda bao 1-0, pengine wachambuzi wetu wengi wanaingia katika kundi hili. Ushindi wa bao 1-0 una alama tatu sawa na ushindi wa mabao 10-0 au ushindi wowote ule
Kama msimu una mechi 10, timu A ikashinda 1-0 katika mechi zote 10, timu B ikashinda 10-0 katika mechi tisa na kupoteza au kutosa sare mchezo mmoja ubingwa utachukuliwa na timu A licha ya kuwa timu B inaweza kuwa imefunga mabao 100!
Falsafa ya Yanga msimu huu ni alama tatu katika kila mchezo, kocha Miguel Gamondi hilo amelifanikisha kwa asilimia 100 mpaka sasa
Post a Comment