Kamwe awaalika mashabiki mechi dhidi ya Pamba Jiji - EDUSPORTSTZ

Latest

Kamwe awaalika mashabiki mechi dhidi ya Pamba Jiji

Kamwe awaalika mashabiki mechi dhidi ya Pamba Jiji


Usikose kuitazama mechi ya YANGA vs PAMBA JIJI Live bure kwenye simu yako download app yetu itakayo kuwezesha kuitazama mechi hii bure kabisa pia ukiwa na app yetu utweza kutazama chanel za AZAM TV na DSTV bure kabisa pia na mechi zote za Nbc premier league na mechi zote za Ulaya kudownload app yetu bonyeza 👉🏻HAPA


 Alhamisi Oktoba 03 2024 Yanga itarudi tena uwanja wa Azam Complex kuikabili Pamba Jiji katika mchezo mwingine wa ligi kuu ya NBC

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema wanakwenda katika mchezo huo wakiwa na tahadhari kubwa lengo likiwa kuzisaka alama zote tatu

Kamwe amesema Pamba jiji wamekuwa na mwenendo usioridhisha msimu huu hivyo anafahamu watachukua tahadhari kubwa katika mchezo dhidi ya Yanga

Msemaji huyo wa Yanga amesisitiza kuwa malengo ya mabingwa hao watetezi ni kuhakikisha wanashinda kila mchezo ili warudi katika nafasi yao

"Tarehe 3, saa 12 jioni tutakuwa uwanja wa Azam Complex kucheza na Pamba Jiji. Utaratibu wetu ni uleule, tujitokeze kwa wingi uwanjani ili kuwaunga mkono wachezaji wetu ambao wanatuhitaji sana"

"Juzi tulicheza saa tatu usiku na mkajitokeza kwa wingi, tunaamini Alhamisi pia mtakuja kwa wingi uwanjani"

"Tunafahamu mchezo dhidi ya Pamba Jiji hautakuwa mwepesi licha ya kunza ligi kwa kusuasua. Mara nyingi timu za aina zinapokutana na Yanga hubadilika na kuonyesha upinzani mkali"

"Lakini sisi tumejipanga na lengo letu kushinda kwani safari yetu ni kuelekea kileleni mwa msimamo wa ligi," alisema Kamwe

Juzi Yanga iliichapa KMC bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex na kusogea hadi nafasi ya nne katika msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 9

Baada ya mchezo dhidi ya Pamba, ligi itasimama kupisha kalenda ya FIFA ambapo mchezo utakaofuata pale ligi itakaporejea ni dhidi ya Simba Oktoba 19

KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA


PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE  HAPA



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz