Dube atupia Zimbabwe ikiichapa Namibia 3-1
Mshambuliaji wa Yanga Prince Dube jana aliifungia bao muhimu timu yake ya Taifa ya Zimbabwe katika mchezo dhidi ya Namibia kuwania kufuzu michuano ya Afcon 2025
Mchezo huo uliopigwa Durban huko Afrika Kusini, uliishuhudia Zimbabwe ikiibuka na ushindi wa mabao 3-1
Dube aliingia katika dakika ya 81 na dakika nane baadae akafunga bao la tatu lililowahakikishia Zimbabwe alama tatu muhimu na kufikisha alama nane kundi J
Zimbabwe iko nafasi ya pili kundi J nyuma ya Cameroon ambao tayari wamefuzu
Mapema Cameroon waliichapa Kenya bao 1-0 katika mchezo ambao kiungo wa Yanga Duke Abuya alianza katika kikosi cha Kenya
Dube na Abuya wamemaliza majukumu ya timu za Taifa na leo wanatarajiwa kurejea nchini kuungana na Yanga inayoendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba utakaopigwa Oktoba 19
Nyota hao wanaungana na Stephane Aziz Ki na Clatous Chama ambao wanatarajiwa kutua nchini wakati wowote baada ya kukamilisha majukumu ya timu za Taifa
Chama hakusafiri na timu ya Taifa ya Zambia kuelekea Chad kutokana na matatizo ya kifamilia
Nyota wengine wa Yanga wanatarajiwa kumaliza majukumu ya timu za Taifa leo
Bakari Nondo Mwamnyeto, Dickson Job, Ibrahim Bacca, Mudathir Yahya na Clement Mzize watakuwa na timu ya Taifa ya Tanzania kuchuana na DR Congo katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Khalid Aucho atakuwa na timu ya Taifa ya Uganda kuchuana na Sudan Kusini huko Juba
Kennedy Musonda atakuwa na timu ya Taifa ya Zambia kuchuana na Chad ugenini wakati Djigui Diarra akiingoza Mali katika mchezo dhidi ya Guinea Bissau ugenini
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
Post a Comment