Kiungo wa Yanga Clatous Chama amesema jambo kubwa analotamani kulifanikisha akiwa na Yanga ni kutwaa taji la ligi ya mabingwa barani Afrika
Chama aliyetua Yanga katika dirisha lililopita la usajili akitokea klabu ya Simba, amefichua kuwa miongoni mwa sababu zilizomfanya atue kwa Wananchi ni pamoja na kiu yake ya kushinda mataji makubwa barani Afrika
"Naweza kusema sababu kubwa kwangu kujiunga na Yanga ilikuwa kufuata changamoto mpya katika maisha yangu ya soka"
"Nina kiu ya kutwaa taji la Afrika. Nilipoitumikia RS Berkane kwa muda mfupi nilifanikiwa kidogo kwani mwishoni mwa msimu waliweza kutwaa kombe la Shirikisho ingawa mimi tayari nikuwa nimeondoka"
"Naamini kwa kujiunga hapa Yanga, naweza kutimiza ndoto hiyo kikamilifu kwa kushirikiana na wenzangu na benchi la ufundi," alisema Chama
Chama pia anafukuzia rekodi nyingine ya ufungaji mabao katika ligi ya mabingwa sasa akiwa na mabao 21
Anahitaji kufunga mabao 10 kufikia rekodi ya Mohammed Aboutrika na Tresor Mputu ambao ni wafungaji bora wa muda wote wa ligi ya mabingwa wakiwa wamefunga mabao 31 kila mmoja
Wachezaji hao tayari wamestaafu huku Chama akiwa bado na misimu kadhaa ya kuifukuzia rekodi hiyo
Post a Comment