Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali amesema sare ya mabao 2-2 dhidi ya Coastal Union sio matokeo waliyoyatarajia lakini lazima kuheshimu matokeo ya mpira wa miguu
Ahmed amekiri Simba haikuwa katika ubora ambao imeonekana katika mechi zilizopita na hiyo inaweza kuwa sababu ya kukosa alama zote tatu katika mchezo huo
'Semaji' amewataka Wanachama na Mashabiki wa Simba kuwa watulivu na kuendelea kuisapoti timu yao kwani mpaka sasa wako njia sahihi katika kutimiza malengo msimu huu
"Nisema tu hatukuwa na mchezo mzuri sana. Ile kasi na ubora tulioonyesha katika mechi zilizopita haikuonekana. Pengine ni presha inayotokana na mahitaji ya timu kushinda kila mechi"
"Sio suala la mchezaji mmoja, nafikiri ni timu nzima haikucheza vizuri, ukisema uchague mchezaji bora wa mechi kutoka upande wetu ni ngumu kumpata"
"Lakini matokeo haya hayapaswi kututoa mchezoni. Huu ni mchezo wa tano, bado tuna safari ndefu katika msimu kwani kuna mechi 25 za kucheza," alisema Ahmed
Mchezo utakaofuata ni dhidi ya Yanga, ukitarajiwa kupigwa baada ya mapumziko ya kalenda ya CAF, Oktoba 19
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
Post a Comment