Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga Simon Patrick amethibitisha mabingwa hao wa nchi kukamilisha mchakato wa kumsajili Yusuph Kagoma mwezi March 2024 kutoka klabu ya Fountain Gate
Akizungumza katika mkutano na wanahabari mapema leo, Simon amesema mazungumzo kati ya Yanga na Fountain Gate kwa ajili ya usajili wa Kagoma yalianza tarehe 03 March 2024
"Yanga ilipewa masharti na Fountain Gate ya kulipa Milioni 30 kumnunua Kagoma. Baada ya makubaliano ya klabu, pande mbili ziliingia mkataba ya mauziano ya mchezaji"
"Mkataba halali ulisainiwa na pande mbili. Yanga ilipaswa kulipa fedha kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza ikamilishwe kabla ya April 30 na Awamu ya pili ikamilishwe kabla ya Juni 30"
"Yanga ililipa fedha zote Milioni 30 April 30 na March 27 2024 Yanga ilimtumia Kagoma tiketi ya ndege kutoka Kigoma kuja Dar es salaam kwa ajili ya mazungumzo"
"Kagoma alisaini mkataba March 28, 2024, mchezaji aliwakilishwa na Mwanasheria wake, Leonard Richard akisaini mkataba wa miaka mitatu"
"Hivyo mpaka sasa Yanga ina mkataba halali na Yusuph Kagoma. Julai 06 2024 Singida FG wakaomba malipo ya Tsh Milioni 30 tuliyofanya kumsajili Kagoma yawe malipo ya Nickson Kibabage aliyekuwa akiitumikia Yanga kwa mkopo"
"Hata hivyo Yanga ikalipa tena Tsh Milioni 30 nyingine kwa ajili ya kukamilisha malipo ya mchezaji Nickson Kibabage na hivyo jumla kuwa imelipa Tsh Milioni 60"
"Septemba uongozi wa mchezaji waliomba kukaa chini na uongozi wa Yanga kumalizana nje ya Kamati na walitakiwa kukamilisha makubaliano ikiwa ni pamoja na mchezaji kuomba radhi lakini jambo hilo halikufanyika"
"Msimamo wa Yanga ni kuomba Kamati ifuate Kanuni kwani mpaka sasa mchezaji Kagoma ana mikataba ya timu mbili. Kamati ilimzuia mchezaji asitumike lakini inashangaza kuona bado mchezaji ameendelea kutumika," alisema Simon
Yanga imeweka hadharani ushahidi wa malipo ya Tsh Milioni 60 kwa Fountain Gate, ushahidi wa tiketi ya ndege ambayo Kagoma alitumiwa kutoka Kigoma kuelekea Dar es saalam kwa ajili ya kusaini mkataba na ushahidi wa mkataba wa miaka mitatu ambao Kagoma alisaini na kuweka dole gumba
Ni wazi sasa ni jukumu la Kamati kuamua, kufuata kanuni au kuomba itumike busara
Post a Comment