Twendeni tukaujaze uwanja wa Mkapa - Ahmed - EDUSPORTSTZ

Latest

Twendeni tukaujaze uwanja wa Mkapa - Ahmed

Twendeni tukaujaze uwanja wa Mkapa - Ahmed


Usikose kuitazama mechi ya SIMBA vs AL AHLI TRIPOLI Live bure kwenye simu yako download app yetu itakayo kuwezesha kuitazama mechi hii bure kabisa pia ukiwa na app yetu utweza kutazama chanel za AZAM TV na DSTV bure kabisa pia na mechi zote za Nbc premier league na mechi zote za Ulaya kudownload app yetu bonyeza 👉🏻HAPA


 Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amesema nguvu ya Wanamsimbazi wote inahitajika siku ya Jumapili katika mchezo wa mkondo wa pili kuwania kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC)

Ahmed amewataka mashabiki wa Simba kununua tiketi kwa wingi kuhakikisha wanaujaza uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo dhidi ya Al Ahli Tripoli

Ahmed amesema wachezaji wanahitaji sapoti ya mashabiki ili kuhakikisha wanashinda na kutinga hatua ya makundi

Msemaji huyo wa Simba amesema yatakuwa makosa makubwa kwa mashabiki wa Simba kuamua kubaki nyumbani wakiamini Simba imemaliza kazi baada ya kupata suluhu ugenini

"Lazima tutambue kwamba huu mchezo bado upo 50% kwa 50%. Atakayechanga vizuri karata zake ndio atakwenda makundi sababu mchezo wa kwanza ulikuwa sare lakini sisi tunayo faida. Kwao walishindwa kutumia faida ya kuwepo mashabiki zao uwanjani, sisi tutaitumia. Mtu asiregeze masikio kwamba tutafuzu kirahisi, mechi hii bado ni mbichi"

"Sisi tusimame na Simba yetu bila kuangalia ukubwa wa shindano. Kila Mwanasimba ajiulize mwenyewe kwanza kushindwa nyumbani kwetu, pili kushindwa kufuzu makundi ya Kombe la Shirikisho. Tuamke sasa kuipambania Simba yetu ili ifuzu makundi"

"Mechi ya kule Libya tuliachia benchi la ufundi na wachezaji wapambane. Mechi ya Septemba 22 ni mechi yetu wote Wanasimba, Jumapili twendeni uwanjani kushangilia timu yetu, tukaipeleke timu yetu makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika."

"Mpaka sasa tupo nyuma goli 2-0 dhidi ya mashabiki wa Al Ahli Tripoli. Goli la kwanza kuujaza uwanja wao wote kwa mashabiki 50,065. Hili kwetu ni deni na sisi kuujaza. Sina hofu na hilo kujaza uwanja wa Mkapa. Wao walijaa na sisi tunapaswa kujaa. Goli la pili mashabiki wote kuvaa jezi za timu yao, na hilo tuna wajibu wa kwenda kusawazisha. Kila Mwanasimba atakayekuja uwanjani anatakiwa kuvaa jezi mpya ya msimu hii," alisema Ahmed

Katika hatua nyingine, Sandaland The Only One wametoa ofa ya punguzo bei ya jezi kuelekea mchezo huo ambapo jezi zitauzwa Tsh 30,000/- katika maduka yote ya Sandaland

"Kwa kutambua kwamba tunapaswa kuvaa jezi za aina moja, mdhamini wetu wa jezi amepunguza bei kwa punguzo maalumu. Jezi zitauzwa Tsh. 30,000 na zinapatikana kwenye maduka ya Sandaland The Only One lakini pia kwa atakayekuja uwanjani na kununua jezi yake ya Tsh. 30,000 atampa zawadi ya tiketi ya mchezo bure"

KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA


PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE  HAPA



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz