Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Juma Mgunda amesema kikosi hicho sasa kimeiva na kipo tayari kuivaa Ethiopia kesho kwenye mchezo huo wa kwanza wa Kundi H, kusaka tiketi ya kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika
Akizungumza kwenye mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika kwenye Uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge, Dar es Salaam, Mgunda alisema wachezaji wameimarika kwa asilimia 80, na kilichobaki ni kumalizika asilimia zilizosalia ili wawe fiti asilimia 100
"Tumeandaa kikosi na wachezaji wako fiti kwa asilimia 80, na tunamalizia kufanya mazoezi leo tayari kuivaa Ethiopia"
"Tumekuwa tukizungumza na vijana juu ya kuwa na utayari wa kuitetea nchi yao na kuiwakilisha vizuri, wanaonekana wako vizuri na tayari kwa mechi hiyo," alisema Mgunda
Akiizungumzia mechi hiyo, alisema lengo walilonalo sasa ni kushinda mchezo huo ili kujiweka kwenye mazingira ya kwenda kucheza tena fainali za AFCON nchini Morocco, kama ilivyokuwa kwa zilizopita nchini Ivory Coast
"Siku zote jambo lolote ukitaka mwisho wake uwe mzuri ni kufanya mambo mapema, umuhimu wa mechi yetu ni kuanza kushinda na kupata pointi tatu nyumbani ili mbele ya safari tuwe kwenye mazingira rahisi ya kufuzu," alisema
Mgunda amesema wanatambua haitokuwa mechi rahisi kwani hata wapinzani wao watakuja wakiwa na akili kama hiyo, hivyo wao makocha na wachezaji itabidi wafanye kazi ya ziada ili kuhakikisha wanafanya kazi kwa vitendo zaidi
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini ( TFF), Cliford Ndimbo, alisema wametangaza viingilio nafuu ili kila Mtanzania apate nafasi ya kuingia uwanjani kuishangilia Stars ambayo imesheheni wachezaji wenye viwango vya juu
Usikose kuitazama mechi hii live bure kupitia simu yako download app yetu itakayo kuwezesha kuitazama mechi hii pia ukiwa na app yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure kudownload app yetu bonyeza 👉🏻HAPA
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
Post a Comment